Showing posts with label BONGO FLAVA. Show all posts
Showing posts with label BONGO FLAVA. Show all posts

HABARI ZAIDI JUU YA KIFO CHA MANGWEAR:


Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.

Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. 

Hussein Original ambaye yupo Pretoria amesema Ngwear na   M to the P  ambaye walikuwa room moja  wamekutwa wamezima   baada  ya  kuzidhisha  madawa  ya  kulevya...

Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki leo jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi amefariki akiwa usingizini.

Akiongea na mwandishi wetu  muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili za kuamka.


Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka na  kuendela na mishemishe yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.

Jonathan  amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair alikuwa amepanga kurudi leo nchini.


Taarifa za kifo cha Ngwair zimepokelewa kwa mshtuko na watu na makampuni mbalimbali nchini yametuma salamu za rambi rambi kupitia kwenye mitandao ya kijamii.


Kilimanjaro Lager ‏
Umeondoka wakati bado tasnia ya muziki inakuhitaji. Pumzika kwa Amani Albert Mangwea “Cowwizy”.


Ndovu Special Malt
R.I.P Albert Mangweir! You will be missed by many Tanzanians. 


Adam Nditi 
Yani siamini Mangwear amefariki dunia nini ilichomkuta #RIP #Mangwair #akaCowbama


Diva ‏
Jamani Ngwair , am in tears now ….. Jamani!. I can’t believe this. I can’t tweet The RIP….. Whyyyyy?

BREAKING NEWS: MWANAMUZIKI WA Hip-Hop ALBERT MANGWAIR AMEFARIKI LEO

Ngwea akiwa na msanii M to the P jana south africa.mtu wa karibu anasema walitakiwa kurudi dar leo lakini waliwakuta wamezima kwenye room wote wawili baada ya kuji overdose madawa ya kulevya na M to the P yupo hoi hospitali
BREAKING NEWS: Mwanamuziki wa Hip-Hop ALBERT MANGWAIR amefariki dunia LEO huko Afrika Kusini katika hospitali ya Hellena Joseph. Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa habari zaidi.........

PROFESA JAY: AJIUNGA CHADEMA:

Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.




Profesa amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CHADEMA na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu. 


Kujiunga rasmi kwa Profesa kwenye chama hicho kunaashiria kuwa huenda akawa na nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015.
Profesa ameamua kuweka wazi uamuzi wake baada ya watu wengi kuanza kumuuliza maswali. “Mmeniuliza sana kwamba mimi ni CHAMA gani jibu litapatikana Muda sio mrefu!! Still in Dodoma STAY TUNED,” alitweet.
Rapper huyo anayejulikana kama mchawi wa rhymes yupo Dodoma pamoja na wasanii wengine akiwemo Lady Jaydee kwa mwaliko wa Sugu

TIMES FM:Kupiga Bongo Flava Mwanzo Mwisho-Soma Tweet yao Hapa

Kwa Kutumia Kilicho chetu , Asili yetu na Muziki wetu leo katika vipindi vyote utaskikia muziki wa nyumbani wa BONGO FLEVA kwa asilimia ubwa

RUGE:MARUFUKU KUPIGA BONGO FLEVA LEO CLOUDS FM

Kasema hivyo baada yakuzungumzia ishu ya Jide na Clouds na kusema ina maamuzi yake na mfano ni leo hakuna kupiga nyimbo za Bongo Flava, kwamba Clouds ina maamuzi binafsi Kwasababu ni redio binafsi so kutopiga nyimbo za Jide ni maamuzi pia...Pia ameongelea kuwa kinacho mfanya lady jay dee Awashutumu ni maswala binafsi tu ikiwemo Band ya Skylight inayomilikiwa na mtangazaji wa Clouds FM kupata umaarufu mkubwa kwa sasa kuliko Band yake ya Machozi Band...So kumfanya Lady Jay Dee kuweweseka,.

Unaweza Kusikiliza mazungumzo hayo hapa chini:

Gadner Afunguka Kuhusu Beef la Mke Wake Lady Jay Dee na Clouds FM

Leo nilipata nafasi ya kuzingumza na Gadan G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki maarufu nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama ni Wosia wake.
Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza Gada G; 
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?

Gadna G: Ni maneno ambayo yametoka moyoni mwake na ni maneno mbayo anajitetea kama msanii, mimi kama Meneja ukiacha pia kama mke wangu naendelea kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport na kujaribu kuzungumza na Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba watu wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa nayo na wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati ila hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa kisabuni.

Hii ni kama vita mmejipangaje..?

Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie naukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya uhasama lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona kama wanamfatilia kulekule ambapo yeye alipo

Nini mlikiona kama chokochoko...?

Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina, ukayaona yale pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia akaona kama unafaidi, mwisho akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.

Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?

Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategamea umma wa Watanzania au hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake.
Jay Dee anapata saport nzuri kutoka Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.

Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?

Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa. Wangeogopa hii leo hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....

Kauli yako ya mwisho ni ipi..?

Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha kweli anaweza kusema sio sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya mwisho ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na kusikia ukweli ili kama wanakosea wasiendelee kukosea wabadilikee….

Mwisho..!
AKIONGEA NA MTANGAZAJI DAN CHIBO MTANGAZAJI WA TBC FM,NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA


Lady Jay Dee "Siku Nikifa Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu:



Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.

Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.

Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.

Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.
Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.

Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.
Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.

Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.
Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.

Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.

Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame
Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.

Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai
Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.

Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.

Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..

Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.
Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.

Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani??
Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??

Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.

Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma??
Roho gani hiyo??

Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu

BIFF LA NEY WA MITEGO NA NIKKI MBISHI LAFIKA PABAYA


Biff linaloendelea kati ya Rapper Nikki Mbishi na Ney wamitego, linaelekea pabaya hali ambayo imefikia kutukanana kupitia katika status za huduma ya Blackberry (BBM), mida hii kupitia kupitia bbm ya Ney wa mitego ameandika status inayoonekana hapa chini
Sababu hasa ya Ney kupandwa na hasira kiasi hiki bado hakijajulikana kwasababu nimejaribu kumtafuta na simu yake haipatikana. kitakachoendelea utakipata hapa as soon as info zikitufikia