Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Mtoto wa Sokoine alipuka


MTOTO mkubwa wa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine, Lazaro Sokoine, ameibuka na kutoa madai mazito ya kutaka mwili wa baba yake ufanyiwe uchunguzi, kubaini chanzo cha kifo chake.

Mbali na kutaka uchunguzi huo, Lazaro pia amemuandikia barua Rais Jakaya Kikwete akielezea mlolongo wa matukio mengi, likiwemo mgogoro wa familia hiyo na kuporwa kwa ardhi na mali zake zingine alizoachiwa na Hayati Sokoine.

Lazaro alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, huku akishusha madai mazito dhidi ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Namelock Sokoine, ambaye ni mdogo wake.

Kwa nini mwili wa Sokoine uchunguzwe?

Akielezea sababu za kutaka mwili wa Sokoine uchunguzwe, Lazaro alisema miezi minne kabla ya kifo chake mwaka 1984 baba yake alienda nchini Cuba wakati Lazaro akiwa masomoni nchini humo; Sokoine alimwambia mwanaye huyo kuwa asishangae kusikia amekufa kwa njia yoyote ile ikiwamo kupigwa risasi kwani kuna watu wanamuwinda.

Alisema baada ya baba yake kumueleza hivyo alihoji sababu ya kuwa na hofu hiyo ambapo Sokoine alijibu kuwa hali ya nchi wakati huo chini ya Mwalimu Julius Nyerere, ilikuwa mbaya kutokana na vita dhidi ya wahujumu uchumi.

Mtoto huyo (pichani) ambaye ana hali mbaya kiuchumi, alisema baba yake aliendelea kumwambia kuwa kutokana na hali hiyo, Mwalimu Nyerere alimuongezea ulinzi kutoka askari wanne hadi 14.

“Baba alikuja Cuba kwa ajili ya sherehe za uhuru wa nchi hiyo na akaniambia maneno hayo mazito nami nikaenda kuongea na walinzi wake ambao ni Mashaka, Kimaro na Kalbert juu ya hofu hiyo ya baba,” alisema Lazaro.

Alisema miezi minne baadaye alipata taarifa ya kifo cha baba yake kupitia Ikulu ya Cuba hali iliyomfanya ayakumbuke maneno ya tahadhari aliyoambiwa juu ya hofu ya kuuawa.

Akieleza sababu nyingine iliyomfanya atake mwili wa baba yake uchunguzwe upya, Lazaro alisema agizo la Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa wakati huo Imran Kombe, kuwataka walinzi wa Sokoine waliokuwa Dodoma watangulie Arusha badala ya kuandamana naye kwenda jijini Dar es Salaam, linatia shaka kwamba kulikuwa na mpango wa kutaka kumuua.

Alisema kutokana na mazingira hayo, amekuwa akitamani sana kuanzisha harakati za kutaka mwili wa kiongozi huyo maarufu uchunguzwe, lakini hali yake kiuchumi ndiyo inayomkwamisha.

“Kwa sasa sina uwezo ila nikipata pesa nitaanzisha mchakato wa kuchunguza kifo cha baba yangu; nimekuwa nikiuliza hili kwa muda mrefu, watu wamenichukia na sasa wananipiga vita hadi ndani ya familia kwa kuhoji suala hilo, mdogo wangu anayeitwa Joseph Sokoine aliyeko ubalozi wa Tanzania nchini Canada aliniambia nisiulizeulize hili suala, wala nisiliingilie kwani siku moja wataning’oa macho au kuniondoa duniani,” anaongeza Lazaro.

Alisema hivi karibuni wakati mwili wa Sokoine ulipozikwa kwenye kaburi jipya kutoka lile la awali, aliiambia familia yake kwamba isifunge milango ya kaburi ili uchunguzi wa mwili wa baba ufanyike.

Hivi karibuni gazeti hili lilipata kuandika taarifa ya mwili wa Sokoine kuzikwa kwenye kaburi jipya baada ya lile la awali kuharibika na kwamba familia ina mpango wa kutaka kuufanyia uchunguzi mwili huo.

Ikumbukwe kuwa wakati wa kifo chake kulikuwa na mjadala mzito, wengi wakidai aliuawa na kwamba kifo chake kilipangwa na mahasimu wake ndani na nje ya serikali ambao walikerwa na operesheni yake ya kupambana na wahujumu uchumi na mali za taifa.

Kwa mujibu wa sheria, mwili ukishazikwa unaruhusiwa kufanyiwa uchunguzi baada ya miaka 30 na mwakani mwili wa Sokoine utafikisha umri wa miaka 30 tangu ulipozikwa na huo utakuwa muda muafaka kwa wana ndugu hao kutaka kujua ukweli wa kifo cha ndugu yao.

Madai ya kuporwa mali

Akizungumzia suala la kuporwa mali na ardhi, Lazaro alisema ameamua kumuandikia barua Rais Kikwete ili aingilie kati kupata haki zake.

Alisema mwaka 1983, akiwa nchini Cuba Sokoine alimkabidhi kiwanja katika eneo la Kunduchi na hati ya kusaini umiliki wa kiwanja hicho ilipelekwa nchini humo na Paraseko Kone, ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Alisema baada ya kumaliza kusaini, Kone alizirejesha hati hizo na kumkabidhi aliyekuwa Mkurugenzi wa Katapila Tanzania kwa wakati huo, Victor Ole Kimesera, ambaye kwa sasa ni Katibu Mtendaji ofisi ya Katibu Mkuu CHADEMA.

Aliongeza kuwa mwaka 1984 alipokuwa kwenye msiba wa baba yake, aliulizia mahala zilipo nyaraka hizo na mama yake alimueleza zilikokuwa na kwamba alipomaliza masomo nchini Cuba alirejea nchini na kukuta kiwanja hicho kimemilikishwa kwa mdogo wake Kilimbe Edward Sokoine.

Alisema baadaye kiwanja hicho kwa kushirikiana na mdogo wake, walikiuza kwa kampuni moja (jina linahifadhiwa), bila ridhaa yake.

“Kwa sasa mimi nina matatizo makubwa hata msaada unaotolewa na serikali kwa familia yetu mimi sijawahi kuupata nakuapia hata gari wananikataza nisisogelee na anayefanya hivi ni mdogo wangu, Namelock,” alisema Lazaro na kuongeza.

“Baba aliniambia kiwanja nimekupatia na pia kuna ng’ombe dume 600 wa kutumia kujengea hicho kiwanja.”

Lazaro alisema kutokana na hali hiyo aliamua kumuandika barua Rais Kikwete Mei 13 mwaka huu na kulazimika kuja jijini Dar es Salaam kujua hatma ya barua yake kama ilishafika mikononi mwa Rais Kikwete.

“Nina mke na watoto wawili hadi hivi sasa mke wangu amerudi kwao kwa kukosa matunzo, maisha ya kulala chini na kukosa chakula yananikabili; ninaleta matatizo haya kwako ili uweze kunisaidia kupata haki zangu zilizotaifishwa ili niondokane na maisha magumu niliyonayo ya kukosa sehemu ya kulala huku nikiwa na watoto wadogo chini ya miaka mitano na kukosa pesa ya kujikimu kimaisha,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Kutokana na madai hayo Tanzania Daima Jumatano iliwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa simu kujua ukweli wa madai hayo.

Mkuu wa mkoa huyo alisema hakumbuki kupeleka fomu kwa Lazaro akiwa masomoni Cuba, lakini alikiri kukutana naye nchini homo.

“Nakumbuka nilikutana na kijana huyo wakati huo akiwa masomoni Cuba ila sikumbuki hilo la kumpelekea fomu ya umiliki wa kiwanja,” alisema Kone.

Kwa upande wake Namelock ambaye ni mbunge wa viti maalumu (CCM) alikiri kuwa kiwanja anachoeleza kaka yake ni haki yake na kwamba kwa sasa kinamilikiwa na watu watatu kwa njia ya ujanja.

“Tumefuatilia bila mafanikio na juzi alipoenda Ikulu nilimwambia afadhali amwandikie barua Rais, na aliandika imefika kwa kuwa msaidizi wa Rais alinipigia, tena ramani ya hicho kiwanja ninayo hadi sasa,” alisema Namelock.”

Sokoine alifariki Aprili 12, 1984 eneo la Wami-Dakawa akiwa njiani kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam

GODBLESS LEMA: MESEJI ILITOKA KWA MKUU WA MKOA

Tarehe 21 /5/2013 Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) L iberatus Sabas ambaye ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha aliongea na waandishi wa habari juu ya shutuma zangu juu ya ujumbe wa maneno mfupi niliopokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Magessa Mulongo siku ya tarehe 25.04.2013 kutoka kwenye namba anayotumia mkuu wa Mkoa namba 0752960276 namba ambayo imesajiliwa kwa jina la Magessa Mulongo kwenda namba 0764150747 namba ambayo imesajiliwa kwa jina la Neema Lema namba ninayo tumia Mimi , ujumbe unaosema “ Umeruka kihunzi cha kwanza nitakuonyesha kuwa mimi ni Serikali , ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi “

Nimesikitishwa na kufedheheshwa sana na taarifa hii ambayo sasa inathibitisha bila mashaka kuwa Jeshi la Polisi Arusha hasa Mkuu wake anatumika na sina shaka kusema kuwa yeye ni KIPEPERUSHI cha Mkuu wa Mkoa , baada ya Mimi kupokea ujumbe huu tarehe 25/4/2013 nilitoa taarifa kwa vyombo vya habari na nia yangu ya kwenda mahakamani juu ya vitisho hivi .

Haya yafuatayo ni maswali ya msingi ninayojiuliza bila kupata majibu sawia kuhusu taarifa ya Jeshi la Polisi na Mtandao wa simu wa Vodacom .
1) Kwani nini Jeshi la Polisi walikataa kuchukua maelezo yangu Mimi juu ya tuhuma hizo nzito dhidi ya Mkuu wa Mkoa ambaye amenitumia meseji kupitia simu yake ya mkononi kama ninavyolalamika ? lakini pia ni muda takribani mwezi umepita tangu nimetoa malalamiko yangu je katika kipindi chote cha mwezi mzima Jeshi la Polisi waliona ni busara kwenda Kampuni ya Vodacom kutafuta mawasiliano yangu na Mkuu wa Mkoa bila hata kuchukuwa maelezo ya mlalamikaji ambaye pia kwa nafasi yake katika Jamii ni Mbunge ?

2) Nilipokuwa rumande Msaidizi wa Mkuu wa Makosa ya Upelelezi Arusha alinifuata na kuniomba nimpe simu yangu, nilimwambia sina nimemwachia Mke wangu na walimtafuta Mke wangu na kumuomba hiyo simu na kumuhakikishia kuwa akiwapa simu wataniachia na kunifutia kesi na Mke wangu aliwajibu kuwa simu alidondosha kwenye gari ya Polisi ile ambayo walinichukua nayo usiku wa siku waliyonikamata , waliita ile gari wakatafuta hiyo simu na walipokosa walichukua pochi ya Mke wangu na kumwaga vitu vyote na kuanza kuitafuta simu na kumpekua , Je Polisi hapa walikuwa wamekusudia nini ?

3) Kwa namna ya kawaida sana ya upelelezi baada ya Polisi na Vodacom kukuta simu ninayotumia imesajiliwa kwa jina lingine katika msingi wa kawaida wa utafiti Kama ambavyo naelewa au kufikiri vyema huyu mwenye Jina hili angetafutwa kwani meseji ilionekana imetoka kwa Magessa Mulongo na imekwenda kwa Neema Lema , lakini aliyekuwa analalamika ni Godbless Lema , je kama Polisi sio Kipeperushi cha Serikali walipata wapi ujasiri wakutoa maelezo waliyotoa wakati kwenye usajili wa mitandao ya simu namba 0764150747 imesajiliwa kwa jina la Neema Lema bila hata kuchukua nafasi ya kumtafuta Neema Lem a kujua ni nani huyo ambaye simu yake inatumiwa na Mtu mwingine ? na ni kwanini Polisi hawakusema kuwa mimi nimedanganya kwani namba hiyo sio yangu ni ya Neema Lema ?

4) Mimi kama mteja ni nayetumia namba 0764150747 nimehiifadhi namba ya Magesa Mulongo 0752960276 kama ( RC ARUSHA VODA) na ndio jina lililokuja na ujumbe wa vitisho katika simu ninayotumia . Vile vile katika barua ya Vodacom kuna maelelzo ambayo ni ya mashaka , kwamba namba ya simu ya Magesa Mulongo ilituma meseji kwenda namba 0764150747 yenye usajili wa jina la Neema Lema kuwa ni kweli kuwa meseji ilitumwa na namba ya Mulongo isipokuwa Center number sio ya Vodacom , swali , kama namba ya Mulongo ni ya Kampuni yao ndio iliyotuma meseji basi hata hiyo center number ni ya kwao kwani kama ingekuwa sio ya kwao Kampuni ya Vodacom isingeweza kuona taarifa zake katika mfumo wake wa mawasiliano na kuzitolea taarifa hivyo kama wameweza kuwa na taarifa zake maana yake ni kuwa mawasiliano hayo yamepita katika mitandao yao ndio maana Kampuni ya Vodacom imepata taarifa za mawasiliano haya na kuyathibitisha kwa Polisi bila hata Kampuni yenyewe kuchuka nafasi ya kumtafuta mlalamikaji na kujua nini kilichotokea kwenye simu yake , lakini vile vile mimi kama mteja sina wakati wa kukagua center number pindi napotumia simu yangu na sijawahi kufanya hivyo na wala sijawahi kuzingatia kwani sio wajibu muhimu katika matumizi ya simu yangu ya mkononi.

5) Wakati Polisi walipoita vyombo vya habari dhana muhimu hapa ilikuwa ni kutaka kumsafisha Mkuu wa Mkoa na ndio maana barua ya Vodacom kwenda Polisi iko kwenye mitandao ya kijamii jambo mabalo Polisi au Vodacom wasingepeswa kufanya hivyo kama kungekuwa hakuna malengo ya kisiasa katika taarifa hii lakini kitendo cha Polisi cha kutoa taarifa bila kuona meseji kutoka katika simu ninayotumia huu ni uhuni mwingine ambapo ni wa msingi kwa Jeshi la Polisi kwani taarifa zinaonyesha kuwa Polisi wote ambao wamekuwa watesaji na waonevu kwa Viongozi wa Upinzani wamekuwa wakipanda vyeo na kupata thamani kubwa machoni kwa Watawala dhalimu na mifano halisi ya wazi iko mingi.

6) Ni dhahiri kwamba zinatumika njia nyingi kumsafisha Mkuu wa Mkoa kwa masilahi ya Serikali . Katika kesi ya uzushi niliyofunguliwa na Polisi ujumbe huu wa meseji utatumika kama ushaidi na mahakama itaona na kufafanua ukweli halisi , hivyo wote wanoangaika wasubiri kwani hivi punde tutakutana mahakamani .

GODBLESS J LEMA ( MP)

26/5/2013

Lipumba akiri kumsaidia Kikwete Uchaguzi 2010

LIPUMBA AIBUA JAMBO ZITO - AKIRI KUMNUSURU KIKWETE UCHAGUZI MKUU MWAKA 2010

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua suala zito akikihusisha chama chake na “kumnusuru” Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu uliopita.

Profesa Lipumba alitoboa siri hiyo katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, alikokwenda kuswali swala ya Ijumaa.

Huku akisisitiza juu ya umuhimu wa mshikamano wa kiimani, Profesa Lipumba alianza kwa kuzungumzia matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, na ushindani mkali wa kisiasa uliokuwapo.

Alisema hawaoni matunda ya jitihada walizofanya kumnusuru Rais Kikwete asishindwe, kwani hata chini ya uongozi wake, Waislamu wameendelea kutothaminiwa.

“Ninyi masheikh mnajua vizuri zaidi hali ya kisiasa ilivyokuwa, kwamba ilibidi zifanyike juhudi za makusudi ili kuokoa jahazi. Lakini pamoja na kuliokoa jahazi, hali halisi inaonyesha mpaka sasa hakuna matunda yoyote yaliyopatikana, na tupo katika mtihani mgumu zaidi,” alisema.

Katika hali ambayo inasemekana ushindi wa Rais Kikwete ulipatikana kwa mbinu, huku wengine wakiituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ilimnusuru mgombea wa CCM, kauli hii ya Profesa Lipumba inadokeza kwamba anajua mkakati zaidi wa kazi ya Tume ya Uchaguzi.

Katika hali isiyo ya kawaida, Profesa Lipumba anaonekana kuhamasisha Waislamu kujipanga akisema “wenzetu wameanza kujipanga” kuelekea 2015.

“Kwahiyo kama Waislamu tunataka kupata haki zetu, kama tunataka kuishi kama raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu, lazima tujipange kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015; na sisi tuanze kujipanga kwa sababu wenzetu wameanza kujipanga, vinginevyo tutaendelea kubaki maskini na raia wa daraja la nne katika nchi yetu wenyewe.

“Mwaka 2010 wakati mshindi wa uchaguzi wa rais alipotangazwa, mimi nilikwenda kwenye hafla ya kutangazwa matokeo, na nilikwenda makusudi tu, siyo kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, ila nilikwenda makusudi kwa kujua hali ya kisiasa ilivyokuwa wakati huo.

“Huku nilikutana na Sheikh Basaleh. Nilipokutana naye, alinipongeza; sijui kama yeye anakumbuka, akaniambia ‘umeweka mbele imani yako na umekuwa mwelewa wa mambo.’”

Hata hivyo, licha ya Profesa Lipumba kuwaambia Waislamu wajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu, hakusema wajipange kupitia chama kipi.

Lakini alisisitiza kwamba uchaguzi ujao ni zaidi ya siasa au rais yupi anafaa, bali maslahi, hasa ya rasilimali nyeti zinazopatikana katika ukanda wa Pwani ya Mashariki, eneo ambalo alisema linakaliwa zaidi na watu wenye imani ya Kiislamu.

Katika moja ya kauli zake, Profesa Lipumba alisema kwamba kuna chama kimoja kinataka kuchukua madaraka ya nchi, lakini kinasaidiwa na mataifa ya magharibi, yasiyoenzi wala kuthamini imani ya Kiislamu.

Kwa muda sasa, zimekuwapo tetesi kwamba CCM imekuwa inafanya siasa za udini dhidi ya vyama vya upinzani, hasa inapoona maslahi yake yapo hatarini.

Mwaka 2010 makada kadhaa wa CCM walitumia mitandao ya simu kuchonga (spoofing) ujumbe wa simu ulioshambulia mgombea mmoja wa upinzani, ukimhusisha na imani yake.

Kauli ya Lipumba imethibitisha pia minong’ono iliyokuwapo muda mrefu kuwa baadhi ya kura za Profesa Lipumba zilipotelea kwa Rais Kikwete.

Katika uchaguzi huo, Lipumba alitangazwa kushika namba ya tatu, nyuma ya Rais Kikwete na Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA.

Alipoulizwa kuhusu ziara yake msikitini na kauli aliyotoa, Profesa Lipumba alikiri kwamba alikwenda kuzungumzia hali ya kisiasa nchini

SIRI YA KIFO CHA KAMANDA WA POLISI LIBERATUS BARLOW YAFICHUKA.

Sasa ni wazi kwamba aliyekuwa kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza ameuawa na genge ndani ya Polisi akiwemo Kamanda Polisi anayejulikana kwa jina la Muna, gazeti la Jamhuri limeripoti katika ukurasa wa Mbele kabisa (Nimesoma kwenye website yao Deo Balile akilalamika gazeti kununuliwa kwa jumla na watu wasiojulikana) 

Kuvuja kwa siri hiyo kumetokana na mmoja wa jambazi sugu ajulikanaye kwa jina la Edward Malele kujisalimisha ktk vyombo vya ulinzi na kutoa siri zote. 

Jambazi huyu aliombwa wa genge ndani ya polisi kushiriki katika mpango wa kumwua kamanda Barlow. Akakataa kwa kuwa aliwahi kumfahamu kwa karibu kamanda Barlow. 

Baada ya kukataa kutekeleza agizo hilo baada ya siku chache alishtakiwa kwa kosa la ujambazi na kuswekwa Rumande.

Akiwa huko ndani ya wiki moja alisikia habari za kifo cha kamanda Barlow. Akajua akina na Muna aliowakatalia wamefanya kazi aliyoikataa yeye. Na alijua yuko mahabusu kwa sababu ya kukataa mradi huo.

Baada ya kukaa huko muda mrefu bila shitaka kueleweka wala mshataki wake huko Lupango walimua kumwaichia. Akagoma kutoka kwa sababu anajua kuwa, kwa kuwa amepelekwa huko ili kuficha siri hivyo, akitoka lazima atauawa. Baada ya muda akaamua kukubali kutoka lupango na kukimbilia kituo cha JWTZ huko Mwanza. 

Huko JWTZ Alijieleza vya kutosha na wanajeshi walimwonea huruma wakampa Nauli na Tsh 10,000/= ya kula njiani ilie aende Bungeni huku wakiwa wamemkabidhi namba za simu za wabunge 2 wa upinzani ili wamsaidie. 

Kutokana na kutokuelewa kwake alipokuwa anashangaa shangaa katika eneo la Bunge, alikamatwa na polisi wanalinda eneo hilo. Polisi hao wakapiga simu Dodoma central na Mwanza. Haraka haraka mwanza wakataka arudishwe mwanza kwa kuwa ni jambazi sugu. 

Hata hivyo, kwa katika kurupushani hiyo taarifa zimeshameshamfikia Pinda na Nchimbi ambapo gazeti linaripoti kuwa Pinda ameagiza kijana huyo apewe ulinzi na asirudishwe Mwanza.

Hata hivyo amepelekwa kusiko julikana. 

Kwa mapana zaidi soma gazeti la Jamhuri KAMA zinanunuliwa kwa kasi na watu wasiofahamika

SOURCE: JAMIIFORUMS

PROFESA JAY: AJIUNGA CHADEMA:

Rapper mkongwe nchini, Joseph Haule aka Profesa Jay amejiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA.




Profesa amekabidhiwa kadi ya uanachama wa CHADEMA na mbunge wa Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu. 


Kujiunga rasmi kwa Profesa kwenye chama hicho kunaashiria kuwa huenda akawa na nia ya kugombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015.
Profesa ameamua kuweka wazi uamuzi wake baada ya watu wengi kuanza kumuuliza maswali. “Mmeniuliza sana kwamba mimi ni CHAMA gani jibu litapatikana Muda sio mrefu!! Still in Dodoma STAY TUNED,” alitweet.
Rapper huyo anayejulikana kama mchawi wa rhymes yupo Dodoma pamoja na wasanii wengine akiwemo Lady Jaydee kwa mwaliko wa Sugu

PICHA ZA MBUNGE MSIGWA ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI IRINGA MCHANA




Mbunge Msigwa akishuka katika gari ya polisi baada ya kufikishwa mahakamani mchana huu



Mbunge Msigwa akishuka katika gari hilo la polisi tayari kwa kuelekea chumba cha mahakama



Mbunge Msigwa akiwa na gazeti mkononi baada ya kufikishwa mahakamani leo



Watuhumiwa wengine wa vurugu za machinga na polisi wakishuka katika karandinga la polisi










Wakili wa Msigwa kulia akiteta jambo nje ya mahakama



Kada wa Chadema Frank Mwaisumbe akiingia na viongozi wengine wa chadema mahakamani hapo huku wafuasi wao wakizuiwa nje ya mahakama



Wafuasi wa Chadema wakiwa wamezuiliwa nje ya viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa wakati mbunge alipofikishwa katika mahakamani mchana huu



Ulinzi mkali kweli kweli ..NA FRANCIS GODWIN

HUYU NDO ASKOFU"BALOZI WA PAPA ALIYEKUSUDIWA KULIPULIWA NA BOMU ARUSHA

Mhashamu Askofu Fransisco Padila, balozi wa Papa aliyekuwa akiendesha ibada ya Uzinduzi wa Parokia ya Mt Joseph Mfanyakazi ya Olasiti Arusha akiondoshwa chini ya ulinzi mkali kutoka eneo mlipuko ulipotokea na kua na kujeruhi zaidi ya watu 70 jana wakati ibada ikiendelea. Kinachodhaniwa kuwa bomu kilirushwa kikiwa kwenye mfuko wa rambo na kisha kulipuka, wakati huo Balozi wa Papa alikuwa anajiandaa kukat utepe kufanya uzinduzi.

Kigwangallah matatani kwa tuhuma za ufisadi



MBUNGE wa Nzega, Dk. Hamisi Kigwangalla (CCM), anadaiwa kuliibia taifa kwa kutumia vibaya misamaha ya kodi ya mamilioni ya shilingi kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha afya eneo la Uchama, wilaya ya Nzega. Kwa mujibu wa nyaraka ambazo Tanzania Daima Jumatano imezipata, Dk. Kigwangallah amejipatia misamaha ya kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wake kupitia kampuni ya Emergent Africa Limited, anayoimiliki kwa asilimia 78 na Bayoun Kigwangallah ana asilimia 22. Kupitia kampuni hiyo, mbunge huyo ameingiza nchini bidhaa mbalimbali ambazo badala ya kuzielekeza katika ujenzi, amefungua duka la kuuza vifaa vya ujenzi eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam na nyingine anaziuza kwa wafanyabiashara wengine.


Nyaraka hizo zinaonyesha kuwa kampuni ya Emergent Africa Ltd, ilisajiliwa katika Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) Septemba 27, 2011 na iliruhusiwa kupata misamaha hiyo kuanzia Septemba 2011 hadi Agosti 2014. Kwa mujibu wa makubaliano kati ya kampuni ya Emergent Afica Ltd na TIC, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliombwa kuisamehe kodi kampuni hiyo ya Dk. Kigwangallah vitu mbalimbali vyenye orodha toka namba 1 hadi 390. Bidhaa hizo kwa uchache ni kompyuta 1042, mashine za kutolea kopi 12, printa 12, ‘binding machines’ 12, vikokotozi (calculator) 640, projekta 12, video kamera 12, feni 30, vifaa vya simu masanduku 28, jenereta moja, magari aina ya Toyota 13, lori 3, Nissan Navarra Pik up 4, Mitsubishi Canter 2 na mabasi madogo manane.


Pamoja na msahama huo, Dk. Kigwangallah kupitia kampuni hiyo, aliingiza nchini vitu bidhaa mbalimbali vikiwemo vigae vya sakafuni 2500 vyenye ukubwa wa 600X600 na 1000 vyenye ukubwa wa 400 X 400 pamoja na vigae vya ukutani. Katika orodha hiyo viko viti na meza za kulia, hema la bustanini, sofa, kabati za kuwekea nguo, mazulia, vitanda na magodoro, televisheni na vingine. Aidha nyaraka hizo zinaonyesha baada ya kupokea bidhaa hizo kutoka nchini China, ziliuzwa katika maduka mbalimbali ya Kariakoo na vigae vingine kuuzwa kwa mkuu wa wilaya moja mkoani Tanga (hatukumtaja) kwa kuwa hakupatikana kujitetea.


Hata hivyo, kumeonekana utata katika nyakara hizo kwani kampuni ya Delmas iliyosafirisha kontena la bidhaa hizo kuja kwa Dk. Kigwangallah, ziko tofauti na ankara za malipo. Ankara hizo zinaonyesha kuwa zilitolewa na makampuni ya Louis Valentino Investment and Development Co. Ltd iliyopo Na. 19 Ji Hua 3 Road Foshan na Sharpeye Furniture. Wakati manunuzi yakionekana kufanyika China Oktoba mosi, 2012, nyaraka nyingine zinaonyesha kuwa mali zilishaingizwa nchini tangu Aprili 14 mwaka huo, kupitia kampuni ya Innovative Freight yenye TIN 100-145-596, risiti namba 2012/0000002986. Na nyaraka za mamlaka ya mapato zinaonyesha bidhaa hizo ziliingia nchini Aprili 3 mwaka jana, hali inayoonyesha kupishana katika tarehe za kununua na kuingiza bidhaa hizo.


Pia utata huohuo unaonekana katika taarifa za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambazo zinaonyesha bidhaa hizo zilikaguliwa Machi 28, 2012. Huku kukiwa na orodha zinazotofautiana za makampuni mawili ya kibiashara wakati ankara ya malipo ilikuwa moja. Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa kontena hilo lilipofika nchini lilionekana kuwa na vitu tofauti na vile vilivyoorodheshwa, hivyo kusababisha kontena hilo kufanyiwa uchunguzi usio wa kawaida kwa kupekua mzigo mmoja mmoja. Dk. Kigwangallah alipotafutwa kwa simu kufafanua tuhuma hizo, alisema amebanwa na kazi. Na alipoambiwa ametumiwa maswali kwenye barua pepe yake, aliahadi kujibu lakini hakufanya hivyo.


Alipopigiwa tena jioni, alisema, “Sema haraka unataka nini?” Alipoulizwa juu ya tuhuma hizo alikata simu. Lakini baadaye aliandika ujumbe kwa simu: “Nitakupigia jioni nikitoka bungeni.”Alipoambiwa inaandikwa habari gazetini, alijibu kwa ujumbe mfupi kuwa tuhuma zilikuwa za uongo bila kufafanua.


Source: Kigwangallah matatani kwa tuhuma za ufisadi. Retrieved from Tanzania Daima

Tuhuma nzito: Chadema yamtuhumu Kinana kuhusika na biashara ya pembe za ndovu

Dodoma. Kambi ya Upinzani Bungeni imetoa tuhuma nzito kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ikidai kuwa anajihusisha na mtandao wa ujangili nchini.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi amejibu tuhuma hiyo akisema ni za uongo huku akiituhumu kambi hiyo kuwa imedanganya wakati inajua ukweli kuhusu tuhuma dhidi ya Kinana.
Akiwasilisha maoni ya upinzani kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2013/14, Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Maliasili, Mchungaji Peter Msigwa alisema vitendo vya ujangili vimekuwa vikilitia doa taifa kwenye jumuiya za kimataifa.
“Kwa bahati mbaya ni kwamba wahusika wengi ambao wanatajwa kwa ushahidi ni makada maarufu na wengine ni viongozi waandamizi wa CCM,” alisema Mchungaji Msigwa.
“Tumeshuhudia watuhumiwa wengine wa ujangili ambao Ikulu imediriki kuwapatia nafasi kubwa za uongozi wa taifa hili, licha ya kutajwa kwenye ripoti ya uchunguzi kuhusiana na ujangili.”
Alisema mwaka 2009, meli ya Kampuni ya Wakala wa Meli ya Sharaf Shipping inayomilikiwa na Kinana ilikamatwa China ikiwa na makontena yenye nyara za Serikali ikiyasafirisha kwenda Hong Kong.
“Nyaraka zilizopo Ofisi za Wakala wa Usajili wa Kampuni na Biashara (Brela), zinaonyesha kuwa kampuni hiyo ya Kinana ilisajiliwa Oktoba 2003 na kupewa hati na. 47221.
“Nyaraka zinaonyesha kuwa Kinana anamiliki hisa 7,500 kati ya 10,000 za kampuni hiyo iliyosajiliwa Dar es Salaam. Mshirika mwenzake katika kampuni hiyo, Rahma Hussein ambaye ni mke wake anamiliki hisa 2,500,” alisema Msigwa.

Dk Nchimbi ajibu mapigo
Akijibu tuhuma hizo, Waziri Nchimbi alisema: “Ukiona mtu anasimama na kuamua kusema kuwa hakuna kinachofanywa na wizara kuhusu masuala ya ujangili, ni wazi uelewa wake unakuwa na utata mkubwa.”
Alisema hoja zilizojengwa dhidi ya Kinana ni uongo mtupu... “Nimejaribu kufuatilia kwa makini alichokisema alikimaanisha, alikielewa, alikitafakari au aliandikiwa tu akaenda kusoma? Baada ya kutafakari kwa kina nikagundua hakuwa na nia mbaya, aliandikiwa tu na ameenda kusoma,” alisema Dk Nchimbi.
Alisema ukweli wa jambo hilo ni kwamba ipo tofauti ya majukumu ya kampuni za Wakala wa Meli na shughuli za kupakia mizigo bandarini huku akituhumu kambi ya upinzani kuwa inajua ukweli lakini imeamua kupotosha umma.
Dk Nchimbi ambaye alikuwa mchangiaji wa kwanza, alisema wakala hawezi kuwa mmiliki wa meli, bali anamwakilisha mwenye meli kwenye shughuli ndogondogo zinazofanyika inapofika nchi fulani kama kuhudumia watumishi wa meli, mahitaji muhimu na kufanya usafi.
“Lakini kuna watu wanaitwa ‘clearing and forwarding (Kupakua na kupeleka mizigo). Napenda kukwambia Mchungaji Msigwa kuwa kazi yao ni kupeleka na kutoa mizigo bandarini,” alisema Dk Nchimbi na kuongeza;
“Kule ndiko kuna utaratibu wa upekuzi, katika utaratibu wa upekuzi mtu wa ‘shipping agency’ (wakala wa meli) hahusiki, sina shaka hata kidogo Mchungaji Msigwa analijua hili ninalolisema, ila amelifumbia macho kwa makusudi kwa masilahi yasiyokubalika katika taifa.”
Alisema kumekuwa na uvumi ambao umekuwa ukifanywa kwa makusudi kuwa Kinana anahusika na meli iliyohusika kusafirisha pembe zile.
“Uvumi huu ni uzushi, meli iliyobeba mizigo ile inaitwa Delmas Nakadha, mmiliki wake anaitwa Bus Herman Ledley jambo hili Kambi ya Upinzani Bungeni inalijua, ila kwa masilahi yasiyokubalika katika taifa wameamua kupotosha Bunge lako,” alisema.
Alisema baada ya uchunguzi wa kutosha, wahusika walibainika na ikafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi namba 3 na 4 ya mwaka 2009 kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.
“Hawa (anawataja) ndiyo waliopelekwa kortini, uchunguzi ulijidhihirisha kuwa ndiyo watuhumiwa wa jambo hili, Kambi ya Upinzani Bungeni inalijua,” alisema


SOURCE: GAZETI LA MWANANCHI

CHEKI SHANGWE YA WATU WA ARUSHA NA MBUNGE WAO SAIVI:



ARUSHA BILA LEMA NI SAWA NA NCHI BILA KATIBA MOJA YA BANGO LILISOMEKA.

KESI YASOMWA KWA DAKIKA 12 KESI YA PIGWA KALENDA KUSIKILIZWA TAREHE 29 MAY 2013. LEMA AWEKEWA DHAMANA NA MTU MMOJA (MWANANCHI WA KAWAIDA TU) YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI MOJA.

WANANCHI WAANDAMANA POLISI WAWAPISHA.

LEMA AWASIHII WAFUASI WAKE WASIMUITE MKUU WA MKOA SHOGA.






OLYMPUS DIGITAL CAMERA


OLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERAOLYMPUS DIGITAL CAMERA

PADRI WA KANISA KATOLIKI HUKO MOSHI AFUMANIWA LIVE NA MKE WA MTU AKIWA UCHI WA MNYAMA

KANISA Katoliki Jimbo la Moshi limeingia katika kashfa nzito baada ya padri wake, Father Urbanus Ngowi wa moja ya parokia zake kudaiwa kufumaniwa na mwanamke anayesemekana ni mke wa mtu

Father Ngowi akiwa ameduwaa baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa mtu aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.
Sakata la fumanizi hilo linadaiwa kutokea Jumatatu ya wiki iliyopita chumbani kwa padri huyo, Marangu Wilaya ya Moshi  Vijijini ambako Father Ngowi inasemekana alikutwa ‘laivu’ akiwa na mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la kijamii la Mama P.

Pamoja na kunaswa huko, vyanzo havijaeleza humo chumbani wawili hao walikuwa wakifanya nini!


Habari zinadai siku ya tukio, mwanamke huyo aliingia nyumbani kwa padri huyo ambapo baadhi ya ndugu wa mumewe walikuwa wakimfuatilia baada ya madai yaliyokuwepo kwamba ana ukaribu wenye maswali mengi na mtumishi huyo wa Mungu.


“Unajua siku nyingi ilivuma kwamba Mama P na Father Ngowi wana ukaribu wenye maswali mengi, mume wake alifuatilia na kubaini ni kweli lakini akashindwa kuutenganisha ukaribu wao,” kilidai chanzo.

Father Ngowi akijaribu kuomba samahani baada ya kufumaniwa.

Chanzo kikaendelea kudai kwamba baada ya kuona mkewe amejikita kwa mtumishi wa Mungu, mumewe alinyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.

Chanzo: Sasa siku hiyo baada ya ndugu wa mume kumfuatilia mpaka anaingia kwa Father Ngowi, wakaona ni bora watafute mpigapicha ili kupata picha za tukio ambazo zitakuwa ushahidi siku za mbele.


“Walipompata wakazama ndani, sekeseke likaanzia hapo. Walimkuta mwanamke huyo na mtumishi wa Mungu wapo kitandani.”

 
Father Ngowi na Mama P wakivaa nguo zao kwa aibu baada ya kufumaniwa.

Habari zinadai kwamba kufuatia tukio hilo, tayari Kanisa Katoliki limemweka kitimoto padri huyo ambaye alikuwa akihudumu katika Parokia ya Korongoni, Moshi Vijijini kabla ya kuhamishwa na kupelekwa Parokia ya Makomu, Marangu ambako inadaiwa ameshushwa cheo.


Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Father Ngowi alikana kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake lakini alipobanwa sana na mabosi wa Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki Moshi, alikiri na kudai ibilisi alimpitia na kuomba kanisa limsamehe na kutompa adhabu kali ambayo itamuathiri kisaikolojia.


Hili ni tukio kubwa na la aina yake kuwahi kulikumba Kanisa Katoliki nchini kwa padri wake kudaiwa kukutwa na mke wa mtu chumbani kwake!

Father Ngowi na Mama P wakiwa na nyuso za aibu baada ya tukio hilo.

Kuna madai kwamba mwaka jana (2012), Father Ngowi, mbele ya waumini wake alisoma barua yenye kukana shutuma zote zilizoelekezwa kwake kwamba amekuwa na ukaribu wenye maswali mengi na wake za watu.


Taarifa zilidai kuwa padri huyo aliweka wazi akisema si kweli kwamba amekuwa na ukaribu unaotajwa, akawataka waumini wake wapuuze tuhuma hizo alizosema  zina mwelekeo wa kuchafua sifa yake na taswira ya Kanisa Katoliki kwa jumla.


Hayo ni madai ya vyanzo vyetu ambavyo viliambatanisha na picha mbalimbali za tukio hilo lenye kushtua waumini sambamba na namba za simu za padri huyo kwa ajili ya mawasiliano ili kujiridhisha.

 Father Ngowi akipatiwa suruali yake.

Source: Global publisher 

LEMA AACHIWA HURU: MJI UMEFURIKA KWA SHANGWE....

MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI ARUSHA IMEMUACHIA KWA DHAMANA MBUNGE WA ARUSHA MJINI KAMANDA GODBLESS LEMA MUDA MFUPI ULIOPITA, VIWANJA VYA MAHAKAMA VILIFURIKA WATU HUKU WAKIWA WAMEBEBA MABANGO YANAYOLAANI KITENGO CHA MBUNGE WAO KUKANDAMIZWA
Kesi imeahirishwa mpaka tarehe May 29, 2013
UMATI WA WATU MAHAKAMANI WAKIFUATILIYA KESI YA LEMA






 

TUNDU LISSU AHOJIWA NA RADIO TEHRAN KUHUSU SAKATA LA KUKAMATWA MBUNGE LEMA




Nchini Tanzania sakata la kukamatwa na kuwekwa mahabusu Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), kwa madai ya uchochezi, limeibua sura mpya baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutajwa kuwa nyuma ya mkakati huo. 

Kwa upande wake Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kimelaani hatua hiyo na kulilaumu jeshi la polisi mkoani Arusha kwa kukandamiza upinzani. 

Chama hicho kimekwenda mbali zaidi na kulituhumu jeshi la polisi Arusha kwamba, limekuwa likitumikia CCM badala ya kutumikia umma. 


Viongozi waandamizi wa CHADEMA wamesema, kutiwa mbaroni Godbless Lema ni mkakati wa CCM wa kukabiliana na nguvu ya chama hicho kikuu cha upinzani ambayo imeteka jimbo la Arusha mjini.

 Salum Bendera amezungumza na Bw. Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni ambaye anaanza kuelezea jinsi chama chao kilivyopokea hatua ya kutiwa mbaroni Mbunge Godbless Lema. 

KUYADOWNLOAD  BOFYA   <<HAPA>>

BAADHI YA MABANGO YALIYOPO MAREKANI YAKIELEZEA UONEVU WA SERIKALI YA TANZANIA

Ukipita kwenye mitaa ya Washington DC katika mtaa wa colombia na 18 street [adams morgan]. Utona kuna mabango na Matagazo kuhusu uonevu unaofanywa na serikali ya Tanzania. Ni picha za akina Mwangosi, Mauaji ya Morogoro, Mauaji kule Songea, na Arusha. Watu wengi wanasema hii Tanzania si inchi ya amani  tena?.Kuna mwingine akasema imebadilika sana. Tunachotakiwa ni kupiga simu au kumweleza congress man wako kuhusu hii issue. Tupate ukweli wake.