Showing posts with label TANZANIA POLITICS. Show all posts
Showing posts with label TANZANIA POLITICS. Show all posts

Ufisadi mkubwa kampuni za simu


KWA UFUPI
“Misamaha kwa kampuni za mawasiliano ni miaka mitano na TIC inaweza kuongeza miaka mingine mitatu. Kutokana na hali hiyo tunahitaji marekebisho ya sheria ili tuweze kuzibana hizi kampuni ziweze kulipa kodi na kuchangia pato la ndani,” alisema Zitto.Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Zitto Kabwe hakuwa tayari kueleza maeneo ambayo Serikali imekuwa ikipunjwa kodi na kampuni hizo na badala yake amesema wameunda kamati ndogo ya watu watatu kwa ajili ya kuchunguza wizi huo.

Kamati hiyo ilibaini madudu hayo baada ya kukutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA).

Akizungumza na waandishi wa habari, Zitto alisema wameitaka TRA kuandika mapendekezo ya kufanyiwa marekebisho ya sheria ya fedha ya 2012, ili iwe na uwezo wa kuhakiki uwekezaji wa kampuni za simu na kufanya ukaguzi wa miradi husika ili kubaini kama inafanana na kodi inayotozwa.

Alisema kampuni hizo zina misamaha mikubwa ya kodi ambayo inatolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) bila kushirikisha wadau mbalimbali na kwamba hivi sasa Serikali inapata Sh300 bilioni tu kwa mwaka kama fedha za mapato ya kampuni hizo.

“Misamaha kwa kampuni za mawasiliano ni miaka mitano na TIC inaweza kuongeza miaka mingine mitatu. Kutokana na hali hiyo tunahitaji marekebisho ya sheria ili tuweze kuzibana hizi kampuni ziweze kulipa kodi na kuchangia pato la ndani,” alisema Zitto.

Zitto alisema mbali na mapendekezo hayo, pia wamemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua misamaha yote ya kodi inayotolewa na TIC ili kujiridhisha kabla ya kutoa uamuzi wa kuendelea nayo ama vinginevyo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe alisema: “Kuna fedha zinakatwa kienyeji tu na kampuni hizi, mfano kwa watu 5 milioni kwa siku wanapata Sh1.8 bilioni, sasa kama kampuni hii itakuwa na wateja zaidi inapata kiasi gani, fedha hizi hazipo katika mlolongo wa ukatwaji wa kodi.

“Pia tutahitaji maelezo ya jinsi mnavyodhibiti meseji za chuki ambazo tunaziona kila siku katika simu zetu, pia kampuni hizi zimekuwa zikibadili majina kila baada ya muda fulani jambo ambalo pia linakosesha nchi mapato.”

TRA na TCRA
Mkurugenzi Mkuu wa TRA, Harry Kitilya alisema kinachowakwamisha ni sheria zilizopo, kwamba wanashindwa kukusanya mapato kwa kuwa kampuni hizo zina misamaha ya kodi.
“Misamaha hii ndiyo inatupa wakati mgumu kukusanya mapato, ila kama sheria hii ya misamaha ya kodi itafanyiwa marekebisho tutaweza kuingia kiasi kikubwa cha kodi,” alisema Kitilya.

Naye Profesa Nkoma alisema ili kuzibana zaidi kampuni za simu kuanzia mwezi Julai mwaka huu utafungwa mtambo maalumu wa kudhibiti mawasiliano (TTMS).
Kuhusu wizi wa mafuta bandarini, Zitto alisema kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja ikiwa ni pamoja na kuhoji wadau mbalimbali wanaohusika na suala hilo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema wizi huo umekuwa ukifanywa kutokana na kuchezewa kwa mabomba (flow meters) ya kupakua mafuta kutoka kwenye meli na kwamba WMA pamoja na TRA wamethibitisha kwamba vipimo hivyo havifai kwani vinasoma tofauti na kiasi cha ujazo wa mafuta.

Aliongeza kuwa kitendo cha kuzuia mashine hiyo kutofanya kazi kumezidisha wizi wa mafuta bandarini, jambo ambalo limesababisha kuongezeka kwa malalamiko.

Alisema katika mazingira hayo mkakati wa Serikali wa kuongeza mapato kupitia vyanzo vya ndani hauwezi kufanikiwa, hivyo wabunge wana wajibu wa kuchukua hatua ili kuhakikisha hali hiyo inafanyiwa kazi.

RAISI KIKWETE: NILIWAHI KUSOMEWA ITIKAFU ILI NIFE

Rais Kikwete alisema hayo juzi katika hotuba yake ya ambayo huisoma kila mwishoni mwa mwezi, kauli ambayo imekuja wakati kukiwa na malalamiko kwamba Serikali imekuwa ikifumbia macho matukio ya uhalifu wenye sura ya uhasama wa kidini.

“Mimi binafsi sibagui, hushiriki shughuli za Waislamu na Wakristo kila ninapoalikwa labda nikose nafasi kwa sababu nyinginezo,” aliongeza Rais Kikwete.

Alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa Kikristo na kwamba amekuwa akipendelea kushiriki zaidi katika shughuli za Kikristo kuliko za Waislamu.
“Naambiwa kuwa niko mwepesi kushiriki maziko ya maaskofu kuliko ya masheikh wanapofariki.

“Kuna misikiti mitatu ya Jijini Dar es Salaam ambayo iliwahi kunisomea itikafu ili nife kwa sababu za kubagua dini yao.
“Katika itikafu hiyo waliwajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,” alieleza Kikwete.
“Nimeshashiriki mazishi ya Masheikh kama nifanyavyo kwa maaskofu na watu mbalimbali Waislamu na Wakristo,” alisema.

Alifafanua pale ambapo hakushiriki mazishi ya sheikh au askofu itakuwa ni kwa sababu ya kubanwa na shughuli nyingine ambazo ni lazima zifanywe na yeye au taarifa ilikuwa ya muda mfupi.
“Waislamu desturi yetu ni kuzika mara mtu anapofariki, hicho ni kikwazo kwangu kushiriki mazishi ya masheikh hasa ikiwa ni nje ya Dar es Salaam kwa sababu ya taratibu za kumsafirisha Rais kutoka mahali pamoja kwenda pengine siyo nyepesi,” alisema Kikwete.

Alisema pia Waislamu wanadai kuwa kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo na Serikali haichukui hatua yoyote ya maana. Alisema imefika mahali viongozi na waumini wa dini hizo kubwa mbili kama hawatakubali kubadili mwelekeo wa sasa basi tunakoelekea ni kubaya
“Nchi yetu tutaivuruga na sifa yake ya miaka mingi ya Waislamu na Wakristo kuishi pamoja kama ndugu itatoweka. Tanzania itaacha kuwa kisiwa cha amani na kuingia katika orodha ya nchi zenye migogoro na hata vita ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kikwete.

Alisema Serikali haifurahishwi na kitendo cha mtu kudhalilisha dini ya mwenzake ndiyo maana wapo wahadhiri wa dini ya Kiislamu na wahubiri wa dini ya Kikristo ambao wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka katika matukio tofauti.
“Vyombo vya usalama vinatambua wajibu wao na kama havitimizi wajibu wao huo utakuwa ulegevu wao na siyo kwamba ni sera na maelekezo yangu au ya Serikali,” alisema Kikwete.

Aliongeza; “Mtakumbuka kuwa mara kadhaa nimewakumbusha wakuu wa mikoa, wilaya na vyombo vya usalama kuacha ajizi katika kutimiza wajibu wao kwenye suala hili.”

Kikwete alisema kuuawa kwa viongozi wa dini na kuchomwa makanisa kusichukuliwe kama Serikali yake imeshindwa kulinda usalama wa raia wake.

“Kama ingekuwa hivyo, tungeshuhudia mauaji ya raia, viongozi wa dini na matukio ya kuchomwa nyumba za ibada yakiwa mengi hapa nchini,” alisema Rais Kikwete.

Ajali ya Jengo la ghorofa lililoanguka

Kikwete alisema sheria zitafuata mkondo kwa waliosababisha kuanguka kwa jengo hilo baada ya uchunguzi unaofanywa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.

Alisema watakaobainika kuhusika watatakiwa kufikishwa mahakamani ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni zao za kuendesha shughuli za ujenzi.

Alitaka mikoa yote nchini kujifunza katika ajali hiyo kwa kufuata kanuni za ujenzi ili kuondokana na maafa yanayoweza kujitokeza

ICHEKI PICHA YA MUUWAJI WA PADRE ZANZIBAR



 Hapo ndio tujue kuwa wenzetu hawabahatishi na hawana siasa kwenye kazi zao proffessional....kazi kweli kweli!!wamehadithiwa tu wamemchora mtu yule yule!!Angalia Mchoro wa Polisi Hapo chini na Ufananishe na mtu Huyu..


Mchoro Uliyotumika Kumpata Muuaji
Source:Jamii Forums

LWAKATARE ATUPWA GEREZANI HADI APRIL 3 BAADA YA KUFUNGULIWA MASHITAKA UPYA

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewafutia kesi ya makosa ya ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka( DPP), Dk Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kuwafutia kesi hiyo washitakiwa kwa sababu hana haja ya kuendelea nayo.

Sambamba na hilo, DPP ilimfungulia kesi ya makosa ya ugaidi upya Lwakatare na Ludovick ambapo kesi hiyo mpya namba Na.6/2013 ambapo imepangiwa kwa hakimu mpya Aloyce Katemana. 

Katika kesi ya ugaidi Na.37/2013 iliyofunguliwa na Jamhuri dhidi ya Lwakatare na wenzake Machi 18 mwaka huu, ambayo ilifutwa saa tatu asubuhi na ambayo ilikuwa imekuja kwa ajili ya Hakimu Mkazi, Emilius Mchauru kuitolea uamuzi wa ama wa kuwapatia dhamana washitakiwa au la, hakimu Mchauru alijikuta akishindwa kutoa uamuzi wake kwa sababu mawakili viongozi wa serikali Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Peter Mahugo waliwasilisha hati hiyo ya DPP chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, ambapo kifungu hicho kina mpa mamlaka DPP, kuifuta kesi yoyote ya jinai muda wowote kabla ya haijatolewa hukumu na uamuzi huo wa DPP haujahojiwa na mtu yoyote.

“Kwa kuwa kesi hii Na.37/2013 ilifunguliwa na upande wa jamhuri MAchi 18 mwaka huu, na leo kesi hii ilikuja kwa ajili ya mahakama kutolea uamuzi wa maombi ya washitakiwa kupatiwa dhamana au la pamoja na maombi mengine…mahakama hii inasema haitaweza kutoa uamuzi wake kwa sababu DPP amewasilisha hati ya kutotaka kuendelea kuwashitaki washitakiwa na hivyo mahakama hii inawafutia kesi washitakiwa wote”alisema hakimu Mchauru.

Baada ya hakimu Mchauru kuwafutia kesi, askari kanzu waliwakamata tena washitakiwa hao na kuwaweka chini ya ulinzi wa gari la polisi na ilipofika saa 4:20 asubuhi, washitakiwa hao wakiwa chini ya ulinzi mkali wa wana usalama waliingizwa tena katika ukumbi namba mbili wa mahakama hiyo mbele ya hakimu mkazi mwingine Aloyce Katemana.

Mawakili Wakuu wa Serikal, Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Wakili Mwanadamizi wa Serikali Peter Mahugo walidai kuwa kesi hiyo nimpya na imepewa Na.6 ya maka huu, ambapo washitakiwa ni Lwakatare na Ludovick wanaotetewa na mawakili wa kujitegemea Profesa Abdallah Safari na Peter Kibatara na kwamba hati hiyo mashitaka ina jumla ya mashitaka manne ambapo shitaka la kwanza linaangukia kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 na makosa matatu yote yanaangukia kwenye Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Wakili Rweyongeza alililata kosa la kwanza ambalo linawakabili washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , na kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o Stopover, wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia sumu kwa lengo la kumdhuru Denis Msaki ambaye ni Mhariri wa habari wa Gazeti la Mwananchi ambalo ni kinyume na kifungu cha 227 cha sheria hiyo.

Wakili Rweyongeza alilitaja kosa la pili kuwa ni la kula njama ambalo pia ni kwaajili ya washitakiwa wote ambalo ni kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki kinyume na kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Shitaka la tatu ni la washitakiwa wote ambapo wanashitakiwa kwa kosa la kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.

Shitaka la nne, Rweyongeza alidai linamkabili Lwakatare peke yake ni kuwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28 mwaka jana, Lwakatare akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka King’ong’o kwa makusudi aliliruhusu kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka hayo.

Hata hivyo Hakimu Katemana alisema washitakiwa hao hawatakiwi kujibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na akaiarisha kesi hiyo hadi Aprili 3 mwaka huu, itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Wakili Kibatala aliomba mahakama isikilize ombi lake alilokuwa akitaka kuliwasilisha, lakini Hakimu Katemana alisema yeye ndiye kiongozi na mawakili wa utetezi, Jamhuri wapo chini yake na akamweleza Kibatala mahakama ni mhimili unaongozwa kwa taratibu zake na nilazima Kibatala azifuate, hivyo, kwa kuwa yeye hakimu ana majukumu mengine, leo hayupo tayari kusikiliza ombi la Kibatala wala ombi la upande wa Jamhuri (lilokuwa linaomba mahakama imruhusu Ludovick aendelee kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya hatua zaidi za kipelelezi,) na kuamuru washitakiwa wapelekwe gerezani. 
Itakumbukwa kuwa Machi 18 mwaka huu, Hakimu Mchauri alitoa fursa kwa washitakiwa ya kukubali au kukanusha mashitaka licha ya Hakimu wa Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi kutokuwa na ruhusa ya kutoa fursa hiyo kulingana na makosa yanayowakabili watuhumiwa na kwa mujibu wa sheria za nchi. Mahakama Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za makosa ya tuhuma za ugaidi.

Baada ya kesi hiyo kuairishwa wafuasi wa CHADEMA na watu wengine wakiwa wamevalia sare walipaza sauti na kusema ‘Peoples Power… hakuna kulala hadi kwanza walale wao’.

Hali iliyosababisha wanausalama waliokuwa wamevalia sare na wale waliovalia kiraia waliokuwa ndani ya kumbi wa kesi ilipokuwa ikiendeshewa kuwataka watu wote watoke ndani ya ukumbi huo haraka ili waweze kuwapitisha washitakiwa, amri ambayo wafuasi hao waliitii bila shuruti.

Msafara wa magari nane ukiongozwa na magari ya jeshi la magereza, polisi waliondoka ndani ya viwanja hivyo kwa ajili ya kuwapeleka watuhumiwa katika gereza la Keko , huku askari wa kikosi cha mbwa wakiwa bado katika eneo la mahakama hiyo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. Hata hivyo, hali ilikuwa ni shwari kwa sababu hakukuwepo na vitendo vya uvunjifu wa amani kwani wafuasi wa CHADEMA waliondoka mahakamani hapo kwa utulivu wa hali ya juu huku wengine wakiangua vilio kwa uchungu.

Mbwa waliokuwepo wakiimarisha ulinzi eneo hilo ni Kino, Pd Kambi Simba, Giro, Pd Roja, Pd Ivo, Pd Undra, Pd Bobi ambao wamepata mafunzo ya kuimarisha ulinzi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Lebanon.

Akizungumza nje ya viwanja vya mahakama baada ya kesi kuahirishwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema kwanza asingependa kuingilia mtiririko wa mahakama na kuwataka waandishi wa habari wamuhoji wakili wa washitakiwa. 

Akasema wao wanafanyakazi za mageuzi kwa ajili ya kuwatetea raia wanyonge na maskini na kwamba kilichompata Lwakatare siyo geni, bali ni mtiririko wa mabavu ya dola dhidi ya wanamageuzi.

Wavuti...

KAMANDA LWAKATARE AACHIWA KWA DHAMANA NA KUKAMATWA KWA MAKOSA MENGINE


Wilfred Muganyizi Lwakatare, akionesha alama ya vidole viwili wakati akipelekwa kizimbani juzi Jumatatu.


Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Muganyizi Lwakatare, muda huu ameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya mashitaka yote yaliyokuwa yanamkabili kufutwa na muda huohuo kukamatwa tene na kufunguliwa mashitaka mengine.

HATIMAYE DEREVA ALIYEGONGA POLICE BAMAGA AKAMATWA




Taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa yule Dereva aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2492 CPL-Elikiza na kutokomea, amekamatwa masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya Bamaga
kwa Mujibu wa kamanda wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani nchini,Kamanda Mohamed Mpinga amesema leo kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.

Kamanda Mpiga ametoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete nyumbani kwa Marehemu,hukoUnunio,kaskazaini mwa jiji la Dar. Rais Kikwete alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha Mume na watoto watatu.

TUNDU LISU ATOA UFAFANUZI JUU YA KUJIFUNGIA CHOONI KUKWEPA WAANDISHI WA HABARI




ZIPO taarifa kwamba Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, wiki iliyopita alijifungia chooni kukwepa waandishi wa habari waliotaka kauli yake juu ya video hatari ambayo inadaiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama hicho, Wilfred Rwakatare, alirekodiwa akieleza njama za uhalifu.

Tundu ambaye ni Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, amesema kuwa maelezo yaliyotolewa kwamba alijificha chooni kwa muda wa saa mbili si kweli, kwani hawezi kufanya hivyo.

“Jamani mimi na umri wangu huu nawezaje kuwakimbia waandishi wa habari? Siku zote mimi nafanya kazi na waandishi wa habari,” alisema Lissu na kuongeza:

“Ofisi yangu pale Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam ina choo ndani, nikiwa ofisini kama mtu yupo nje wala hawezi kujua kama mimi nipo chooni. Nadhani hizo taarifa za kusema nilijifungia chooni ni za upotoshaji.

“Halafu haiwezekani mimi nikimbie suala la Rwakatare kwa sababu tayari nilishalitolea maelezo. Mpaka sasa, mimi kama mmoja wa mawakili wanaomtetea, nina maswali yangu kwa jeshi la polisi, kwani ile video haioneshi uhalifu wowote ambao umetendeka.

“Ni kweli niliweka miadi ya kuzungumza na waandishi lakini nilisahau. Nakumbuka jioni kabisa ya siku hiyo, nilipokea SMS ya mwandishi, akiniambia alikaa sana Ofisi Ndogo za Bunge, Dar es Salaam mpaka akachoka, kwa hiyo alishindwa kuniona.”

Wikiendi iliyopita, iliripotiwa na mitandao mbalimbali pamoja na gazeti moja la kila siku kwamba Lissu alijificha chooni kwa saa mbili kukwepa kuonana na waandishi wa habari, waliotaka ufafanuzi wake kuhusu kile kinachoendelea juu ya kesi inayomkabili Rwakatare ambaye ni Kiongozi Mstaafu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

RAIS KIKWETE AENDA KUTOA POLE KWA FAMILIA YA ASKARI ALIYEKUFA KWA AJALI BARABARANI

Taarifa tulizozipata zinaeleza kuwa yule dereva aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2493 CPL-Elikiza Lokisa Nko na kutokomea, amekamatwa juzi usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya Bamaga mapema jana mchana.

Kwa Mujibu wa Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani nchini, Kamanda Mohamed Mpinga alisema jana kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo aina ya Landlover Discovery rangi nyeusi limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.

Kupatikana kwa gari hilo kumekuja baada ya Polisi kufuatilia na kujua mmiliki wa gari hilo kuwa ni kanisa la TAG chini ya Mchungaji Wambura, ambaye kwa ushirikiano alioutoa dereva aliyetambuliwa kama Jackson Stephen, alijulikana na hatimaye kupatikana

Kamanda Mpiga alitoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana jioni nyumbani kwa Marehemu hukoUnunio kiasi cha kilomita 25 hivi Kaskazini mwa jiji la Dar.

Rais Kikwete pamoja na uongozi wa juu wa jeshi la polisi walifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha Mume na watoto watatu. Mume wa marehemu pia ni askari polisi.

Pichani juu Rais Kikwete akimfariji mume wa marehemu na watoto wake pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema.

ULINZI MKALI SHEREHE YA KUTAWAZWA KWA PAPA FRANCIS 1 JIJINI ROME.

Papa Francis akisalimiana na Rais wa Argentina, Cristina Fernandez de Kirchner alipowasili Vatican, jana kuhudhuria sherehe za kutawazwa kwa mkuu huyo wa Kanisa Katoliki zitakazofanyika leo. Picha na AFP.


Vatican City. Ulinzi mkali umeandaliwa kwa viongozi mbalimbali wa kiserikali na wale wa kidini duniani waliowasili jijini Vatican, kwa misa maalumu ya kutawazwa kwa Papa Francis leo.


Waumini na wageni milioni moja akiwamo Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk James Msekela, wanatarajiwa kuhudhuria misa hiyo itakayofanyika kwenye Viwanja vya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.


Baada ya Papa Francis kutawazwa, ataanza rasmi kazi ngumu ya kuliongoza Kanisa Katoliki lenye waumini wengi na ambalo limekumbwa na mizozo kadhaa ikiwamo ya utovu wa nidhamu kwa baadhi ya makasisi.


Kiongozi huyo alichaguliwa Jumatano iliyopita kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Papa Benedict XVI, aliyejiuzulu Februari 28, mwaka huu.

RIPOTI MAALUMU TOKA MAHAKAMA YA KISUTU ALIKOSHITAKIWA LWAKATARE WA CHADEMA



HATIMAYE Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Dk Eliezer Feleshi amemfikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare na mwenzake kwa makosa ya ugaidi.


Mbali na Lwakatare mshitakiwa mwingine ni Ludovick Rwezaula Joseph ambao wanatetewa na mawakili wa kujitetemea Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Nyaronyo Kicheere.


Washitakiwa hao wakifikishwa jana saa mbili asubuhi mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu walikuwa wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Ilala, Duwani Nyanda na kuifadhiwa nyuma ya jengo la mahakama hiyo tayari kwaajili ya kufikishwa kizimbani kosomewa mashitaka yanayowakabili.


Washitakiwa hao waliingizwa ndani ya ukumbi namba moja wa mahakama hiyo saa 7:06 mchana chini ya ulinzi mkali wa wanausalama , huku Lwakatare akiwasalimu wafuasi wa Chadema, kwa kuwaonyesha ishara ya vidole viwili ambapo wafuasi hao walikuokuwa wamefurika mahakamani hapo tangia asubuhi jana wakimjibu kwa kumuonyeshea ishara ya



vidole viwili juu.


Baada ya kupanda kizimbani, jopo la mawaikili wakuu wa seriakali linaloongozwa na Mwanasheria Kiongozi wa Serikali Kanda ya Dar es Salaam, Ponsian Lukosi, Purdence Rweyongeza na Peter Mahugo ambapo walidai hati ya mashitaka ina jumla ya makosa manne.


Wakili Rweyongeza alililata kosa la kwanza ambalo linawakabili washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , na kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o Stopover, wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia sumu kwa lengo la kumdhuru Denis Msaki ambaye ni Mwanahabari wa Gazeti la Mwananchi ambalo ni kinyume na kifungu cha 227 cha sheria hiyo.


Wakili Rweyongeza alilitaja kosa la pili kuwa ni la kula njama ambalo pia ni kwaajili ya washitakiwa wote ambalo ni kinyume na kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki kinyume na kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.


Aidha alilitaja kosa la tatu kuwa ni kutenda kufanya mkutano wa kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.


Wakili Rweyongeza alilitaja shitaka la nne ambalo linamkabili Lwakatare peke yake ni aliwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28 mwaka jana, Lwakatale akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka King’ong’o kwa makusudi aliliruhusu kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka hayo.


Wakili Rweyongeza alidai kuwa makosa hayo yameletwa chini ya sheria mbili tofauti yaani kosa la kwanza linaangukia katika sheria ya Kanuni ya Adhabu lakini kosa makosa yaliyosalia yanaangukia kwenye Sheria ya Kuzuia ugaidi na kwamba makosa yanaoangukia kwenye sheria ya ugaidi huwa hayana dhamana na kwamba ni Mahakama Kuu peke ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.


Wakili Rweyongeza aliieleza mahakama kuwa jamhuri inawasilisha ombi la pili ambapo wanaiomba mahakama imruhusu mshitakiwa wa pili(Ludovick) aende kukaa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kwasababu Jeshi la polisi linamuiitaji kwaajili ya hatua za kiupelelezi zaidi.


Hata hivyo mawakili wa utetezi Peter Kibatara aliomba mahakama iwapatie wateja wake dhamana na kwamba suala la washitakiwa kupatiwa dhamana au kunyimwa ni la mahakama.


Kwa upande wake wakili Lissu alidai aliita hati ya mashitaka kuwa ni kipande cha karatasi kilichowasilishwa na DPP-Dk Feleshi ambacho akionyeshi nembo ya serikali, mhuri na wala hiyo hati ambayo aliipachika jina la kipande cha karatasi kuwa hakikuletwa mahakamani hapo kwa ridhaa ya DPP na kwamba anaiomba mahakama hiyo isiiamini hicho kipande cha karatasi kuwa ni nyaraka halali ya serikali..


Kwa upande wake wakili Profesa Abdallah Safari aliomba mahakama irejee kesi za kupambikiwa zilizowai kufunguliwa mahakamani hapo na ofisi ya DPP miaka ya nyuma ikiwemo kesi ya mauji ya fundi majeneza wa Manzese ya mwaka 2002, iliyofunguliwa na jamhuri dhidi ya Sheikh Issa Ponda na Sheikh Kundecha ambapo yeye alikuwa akiwatetea washitakiwa hao ambapo alilazimika kwenye kuonana na DPP wa wakati huo ambaye ni Jaji mstaafu kwa sasa Juxon Mlai na kumueleza kuwa kesi ile ya mauji ni ya kubambikwa ambapo Mlai alitumia mamlaka yake kuifuta kesi ile.


“Katika kesi hii ya Lwakatare ninachokiona ni matumizi mabaya ya sheria na wale waliombakizia kesi Lwakatare wanastarehe na kufurahi kuona Lwakatare anaenda kuishi gerezani”alidai Profesa Safari.


Akipangua hoja za mawakili hao wa utetezi, wakili wa serikali Rweyongeza alidai kuwa hoja hizo tatu zilizowasilishwa na mawakili wa utetezi ni dhaifu na kwamba anaomba mahakama isiione kesi hii ni ya macho ya chama fulani ya kisiasa, tunaomba mahakama itambue kuwa kesi hii imefunguliwa na upande wa jamhuri na wala haijafunguliwa na chama cha siasa.


Kuhusu hoja ya kuwabambikizia kesi washitakiwa hao,Rweyongeza ambaye alikuwa akionyesha kujiamini alidai kesi hiyo siyo ya kubambikiziwa na kwamba ofisi ya DPP inafanyakazi yake kwa mujibu wa sheria na haipo kwaajili ya kubambikia watu kesi na kwamba kama Profesa Safari anaushahidi Lwakatare kabambikiwa kesi basi aende kuonana na DPP na ampatie huo ushahidi unaonyesha washitakiwa wamebambikiwa kesi.


Akiijibu hoja ya Lissu kuwa DPP amewasilisha kipande cha karatasi kisicho na kibali cha DPP, wakili Rweyongeza alimtaka Lissu aache kasumba ya kuongea mambo bila ya kufanya utafiti kwani DPP amefungua kesi hiyo na amewasilisha kibali chake mahakamani hapo ambapo wakili huyo aliklitoa kibali hicho kama kielelezo hali iliyofanya watu kuanza kuangua vicheko.


Aidha kuhusu hoja ya kutaka washitakiwa wapatiwe dhamana, wakili Rweyongeza alidai kuwa sheria ya ugaidi imetungwa na bunge na bunge ambapo kifungu cha 49 cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi kinakataza kabisa mshitakiwa anayeshtakiwa kwa makosa yanayoangukia kwenye sheria ya ugaidi kupewa dhamana na kwamba washitakiwa hao makosa yanayowakabili yanaangukia kwenye ya ugaidi hivyo mahakama haiwezi kuwapa dhamana.


“Sasa nawashangaa hawa mawakili wa washitakiwa leo hii wanajifanya hawajui matakwa ya kifungu cha 49 cha sheria ya ugaidi kinasema nini.Sheria ya ugaidi imetungwa na bunge hivyo ni sheria halali na kama mawakili wa utetezi wanaona sheria hiyo ni mbaya basi haraka sana nawashauri waende mahakama kuu wafungue kesi ya kikatiba ya kupinga kifungu hicho cha sheria ya ugaidi lakini kwasasa sisi tunasema sheria ya ugaidi ipo kihalali na ndiyo imetumika kuwashitaki washitakiwa hawa”alidai wakili Rweyongeza.


Kwa upande wake hakimu mkazi Emilius Mchauru alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili na kwamba atatolea uamuzi kesho na kuamuru washitakiwa wote wapelekwe gerezani

KIBAKI congratulates UHURU KENYATTA for becoming the fourth President of Kenya


Sunday March 10, 2013 - President Mwai Kibaki has congratulated President -elect Uhuru Kenyatta for becoming the fourth President of Republic of Kenya.



In a statement to media houses on Saturday, the Head of State, who is leaving office after serving two five-year terms, wished Uhuru Kenyatta- success as he prepared to take over leadership.
"To Honourable Uhuru Kenyatta who has been declared President Elect by the IEBC, I express my most sincere congratulations. I wish him best wishes, success and God’s blessings in the noble duty of governing our great country," Kibaki said in the statement.
Kibaki said he was happy with the way IEBC conducted the “most free and fair election in our nation’s history”.
"I commend the entire Independent Electoral and Boundaries Commission, led by the Chairman Isaack Hassan for their diligence and commitment. I also salute our security officials and public servants for their vigilance, hard work and sacrifice," Kibaki said.
He also thanked Kenyans for their patience as the IEBC tallied votes after Monday's election.
"I heartily commend you for exhibiting a great degree of tolerance and patience. I thank you for heeding to my call that we should conduct ourselves in a manner that shows that our democracy has come of age. The peaceful conducting of elections is a victory for Kenya.
"By casting your votes you exercised your democratic right and lived up to your date with destiny. Across our country we have a new crop of leaders who will see to it that we have functional governments at both the county and national levels."
He also promised to oversee a smooth transmission of power to Uhuru Kenyatta on March 26.
"On my part, I commit myself to the management of a smooth transition to the new leadership that the Kenyan people have placed in office. We have credible institutions that should deal with any matter that may have arisen during the electoral process.
"In the meantime, I appeal to Kenyans to be peaceful and calm and allow for any disputes that may have arisen to be resolved within the legal mechanism… after the elections, let us all embrace one another in the spirit of one Kenya one nation. Let us immediately get down to the work of entrenching the economic, social and democratic gains that our nation has made," Kibaki said.