UNAJUA ALICHOKIANDIKA KIBANDA LEO FB????GONGA HAPA



Ufisadi mkubwa kampuni za simu


KWA UFUPI
“Misamaha kwa kampuni za mawasiliano ni miaka mitano na TIC inaweza kuongeza miaka mingine mitatu. Kutokana na hali hiyo tunahitaji marekebisho ya sheria ili tuweze kuzibana hizi kampuni ziweze kulipa kodi na kuchangia pato la ndani,” alisema Zitto.Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Zitto Kabwe hakuwa tayari kueleza maeneo ambayo Serikali imekuwa ikipunjwa kodi na kampuni hizo na badala yake amesema wameunda kamati ndogo ya watu watatu kwa ajili ya kuchunguza wizi huo.

Kamati hiyo ilibaini madudu hayo baada ya kukutana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Mamlaka ya Bandari (TPA) na Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA).

Akizungumza na waandishi wa habari, Zitto alisema wameitaka TRA kuandika mapendekezo ya kufanyiwa marekebisho ya sheria ya fedha ya 2012, ili iwe na uwezo wa kuhakiki uwekezaji wa kampuni za simu na kufanya ukaguzi wa miradi husika ili kubaini kama inafanana na kodi inayotozwa.

Alisema kampuni hizo zina misamaha mikubwa ya kodi ambayo inatolewa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) bila kushirikisha wadau mbalimbali na kwamba hivi sasa Serikali inapata Sh300 bilioni tu kwa mwaka kama fedha za mapato ya kampuni hizo.

“Misamaha kwa kampuni za mawasiliano ni miaka mitano na TIC inaweza kuongeza miaka mingine mitatu. Kutokana na hali hiyo tunahitaji marekebisho ya sheria ili tuweze kuzibana hizi kampuni ziweze kulipa kodi na kuchangia pato la ndani,” alisema Zitto.

Zitto alisema mbali na mapendekezo hayo, pia wamemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua misamaha yote ya kodi inayotolewa na TIC ili kujiridhisha kabla ya kutoa uamuzi wa kuendelea nayo ama vinginevyo.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo Filikunjombe alisema: “Kuna fedha zinakatwa kienyeji tu na kampuni hizi, mfano kwa watu 5 milioni kwa siku wanapata Sh1.8 bilioni, sasa kama kampuni hii itakuwa na wateja zaidi inapata kiasi gani, fedha hizi hazipo katika mlolongo wa ukatwaji wa kodi.

“Pia tutahitaji maelezo ya jinsi mnavyodhibiti meseji za chuki ambazo tunaziona kila siku katika simu zetu, pia kampuni hizi zimekuwa zikibadili majina kila baada ya muda fulani jambo ambalo pia linakosesha nchi mapato.”

TRA na TCRA
Mkurugenzi Mkuu wa TRA, Harry Kitilya alisema kinachowakwamisha ni sheria zilizopo, kwamba wanashindwa kukusanya mapato kwa kuwa kampuni hizo zina misamaha ya kodi.
“Misamaha hii ndiyo inatupa wakati mgumu kukusanya mapato, ila kama sheria hii ya misamaha ya kodi itafanyiwa marekebisho tutaweza kuingia kiasi kikubwa cha kodi,” alisema Kitilya.

Naye Profesa Nkoma alisema ili kuzibana zaidi kampuni za simu kuanzia mwezi Julai mwaka huu utafungwa mtambo maalumu wa kudhibiti mawasiliano (TTMS).
Kuhusu wizi wa mafuta bandarini, Zitto alisema kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja ikiwa ni pamoja na kuhoji wadau mbalimbali wanaohusika na suala hilo ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema wizi huo umekuwa ukifanywa kutokana na kuchezewa kwa mabomba (flow meters) ya kupakua mafuta kutoka kwenye meli na kwamba WMA pamoja na TRA wamethibitisha kwamba vipimo hivyo havifai kwani vinasoma tofauti na kiasi cha ujazo wa mafuta.

Aliongeza kuwa kitendo cha kuzuia mashine hiyo kutofanya kazi kumezidisha wizi wa mafuta bandarini, jambo ambalo limesababisha kuongezeka kwa malalamiko.

Alisema katika mazingira hayo mkakati wa Serikali wa kuongeza mapato kupitia vyanzo vya ndani hauwezi kufanikiwa, hivyo wabunge wana wajibu wa kuchukua hatua ili kuhakikisha hali hiyo inafanyiwa kazi.

Nauli ni Kiama: Sumatra yapandisha nauli za daladala, mabasi ya mikoani, treni na meli


DAR ES SALAAM
 Mamlaka ya Udhibiti wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imepandisha nauli za daladala, mabasi ya kwenda mikoani, usafiri wa reli na tozo za majini kuanzia Aprili 12, mwaka huu.Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Ahmad Kilima alisema jana kuwa nauli za daladala zimeongezeka kwa asilimia 24.46 kwa kuzingatia maoni ya wadau na gharama za uendeshaji.

Kwa upande wa usafiri wa daladala nauli zimepanda kwa umbali tofauti kutoka Sh300 hadi 400, Sh350 hadi 450, Sh500 hadi 600, Sh650 – 750 na kwa wanafunzi kutoka Sh150 hadi 200 katika sehemu yoyote watakayokwenda.

Nauli za usafiri wa mabasi makubwa ya masafa marefu nauli hizo zimeongezeka kwa viwango tofauti. Mathalan kwa basi la kawaida kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya ni Sh30,700, njia ya vumbi kutoka Kigoma hadi Sumbawanga Sh25,400 na basi la hadhi ya kati (Semi Luxury) kati ya Dar na Mwanza ni Sh61,400, wakati basi la hadhi ya juu (Luxury) kati ya Dar na Arusha ni Sh 36,000.

Kilima alisema: “Kuanzia Aprili 12 mwaka huu, kati ya kilometa 0 hadi 10, nauli ya daladala itakuwa Sh400 badala ya Sh300 zinazolipwa hivi sasa.
“Pia nauli za mabasi ya kwenda mikoani zimeongezeka kwa asilimia 20.3 kwa mabasi ya kawaida, mabasi ya kati kwa asilimia 16.9 na mabasi ya daraja la juu kwa asilimia 13.2,” alisema.

Kilima alisema nauli za mabasi ya mikoani zimepanda kutoka Sh30.67 hadi Sh36.89 kwa kilometa kwa mabasi ya daraja la kawaida katika njia za lami.
Kwa upande wa mabasi ya kawaida kwa njia ya vumbi imepanda kutoka Sh37.72 hadi Sh 46.11 kwa kilometa na kwamba mabasi ya hadhi ya kati, nauli zimepanda kutoka Sh45.53 hadi Sh 53.22 kwa kilometa.

Alisema mabasi ya hadhi ya juu nauli zimepanda kutoka Sh51.64 hadi Sh58.47 kwa kilometa.
“Kupanda kwa nauli kunatakiwa kwenda sambamba na huduma bora na kwamba Sumatra imepiga marufuku kutumia wapigadebe kuuza tiketi za safari”alisema.

Usafiri wa Reli
Katika uamuzi huo, usafiri wa reli pia umepanda ambapo daraja la kwanza Dar es Salaam hadi Morogoro, nauli mpya na ya zamani katika mabano ni Sh21,100, (Sh16,852), Dar hadi Dodoma Sh34,700, (Sh27,788), Dar es Salaam-Tabora Sh54,800, (Sh43,859).
Dar es Salaam-Isaka Sh62,100, (Sh49,662), Dar- Shinyanga Sh65,300 (Sh52,229) Dar –Mwanza Sh74,800 (Sh 59,818), Dar- Kigoma Sh75,700, (Sh60,599)

Daraja la pili, Dar es Salaam-Morogoro Sh16,600, (Sh13,280), Dar es Salaam-Dodoma Sh26,400 (Sh 21,092), Dar es Salaam-Tabora Sh40,500 (Sh 32,364), Dar es Salaam-Isaka Sh45,800, (Sh36,605), Dar es Salaam-Shinyanga Sh48,000 (Sh38,390), Dar es Salaam- Mwanza Sh54,700 (Sh43,747), Dar es Salaam-Kigoma Sh55,400 (Sh44,305).

Daraja la tatu, dar es Salaam-Morogoro Sh8,800 (Sh6,138), Dar es Salaam-Dodoma Sh13,500 (Sh9,374), Dar es Salaam-Tabora 20,400 (Sh14,173), Dar es Salaam-Isaka Sh22,800 (Sh15,847), Dar es Salaam –Shinyanga Sh24,000 (Sh16,628), Dar es Salaam-Mwanza Sh27,200 (Sh18,860), Dar es Salaam- Kigoma Sh27,500 (Sh19,084).

Akizungumzia tozo za majini, Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mamlaka hiyo imeridhia ongezeko la tozo la asilimia 34.3 kwa vyombo vinavyotumia bandari za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Alisema awali TPA walipendekeza tozo hizo kuongezeka kati ya asilimia saba hadi 400 kulingana na aina ya huduma zinazotolewa kwa meli zinazotumia bandari za mamlaka hiyo

RAISI KIKWETE: NILIWAHI KUSOMEWA ITIKAFU ILI NIFE

Rais Kikwete alisema hayo juzi katika hotuba yake ya ambayo huisoma kila mwishoni mwa mwezi, kauli ambayo imekuja wakati kukiwa na malalamiko kwamba Serikali imekuwa ikifumbia macho matukio ya uhalifu wenye sura ya uhasama wa kidini.

“Mimi binafsi sibagui, hushiriki shughuli za Waislamu na Wakristo kila ninapoalikwa labda nikose nafasi kwa sababu nyinginezo,” aliongeza Rais Kikwete.

Alisema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa Kikristo na kwamba amekuwa akipendelea kushiriki zaidi katika shughuli za Kikristo kuliko za Waislamu.
“Naambiwa kuwa niko mwepesi kushiriki maziko ya maaskofu kuliko ya masheikh wanapofariki.

“Kuna misikiti mitatu ya Jijini Dar es Salaam ambayo iliwahi kunisomea itikafu ili nife kwa sababu za kubagua dini yao.
“Katika itikafu hiyo waliwajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova,” alieleza Kikwete.
“Nimeshashiriki mazishi ya Masheikh kama nifanyavyo kwa maaskofu na watu mbalimbali Waislamu na Wakristo,” alisema.

Alifafanua pale ambapo hakushiriki mazishi ya sheikh au askofu itakuwa ni kwa sababu ya kubanwa na shughuli nyingine ambazo ni lazima zifanywe na yeye au taarifa ilikuwa ya muda mfupi.
“Waislamu desturi yetu ni kuzika mara mtu anapofariki, hicho ni kikwazo kwangu kushiriki mazishi ya masheikh hasa ikiwa ni nje ya Dar es Salaam kwa sababu ya taratibu za kumsafirisha Rais kutoka mahali pamoja kwenda pengine siyo nyepesi,” alisema Kikwete.

Alisema pia Waislamu wanadai kuwa kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo na Serikali haichukui hatua yoyote ya maana. Alisema imefika mahali viongozi na waumini wa dini hizo kubwa mbili kama hawatakubali kubadili mwelekeo wa sasa basi tunakoelekea ni kubaya
“Nchi yetu tutaivuruga na sifa yake ya miaka mingi ya Waislamu na Wakristo kuishi pamoja kama ndugu itatoweka. Tanzania itaacha kuwa kisiwa cha amani na kuingia katika orodha ya nchi zenye migogoro na hata vita ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kikwete.

Alisema Serikali haifurahishwi na kitendo cha mtu kudhalilisha dini ya mwenzake ndiyo maana wapo wahadhiri wa dini ya Kiislamu na wahubiri wa dini ya Kikristo ambao wamekamatwa na kufunguliwa mashtaka katika matukio tofauti.
“Vyombo vya usalama vinatambua wajibu wao na kama havitimizi wajibu wao huo utakuwa ulegevu wao na siyo kwamba ni sera na maelekezo yangu au ya Serikali,” alisema Kikwete.

Aliongeza; “Mtakumbuka kuwa mara kadhaa nimewakumbusha wakuu wa mikoa, wilaya na vyombo vya usalama kuacha ajizi katika kutimiza wajibu wao kwenye suala hili.”

Kikwete alisema kuuawa kwa viongozi wa dini na kuchomwa makanisa kusichukuliwe kama Serikali yake imeshindwa kulinda usalama wa raia wake.

“Kama ingekuwa hivyo, tungeshuhudia mauaji ya raia, viongozi wa dini na matukio ya kuchomwa nyumba za ibada yakiwa mengi hapa nchini,” alisema Rais Kikwete.

Ajali ya Jengo la ghorofa lililoanguka

Kikwete alisema sheria zitafuata mkondo kwa waliosababisha kuanguka kwa jengo hilo baada ya uchunguzi unaofanywa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.

Alisema watakaobainika kuhusika watatakiwa kufikishwa mahakamani ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni zao za kuendesha shughuli za ujenzi.

Alitaka mikoa yote nchini kujifunza katika ajali hiyo kwa kufuata kanuni za ujenzi ili kuondokana na maafa yanayoweza kujitokeza

Breaking News: Mgodi wafukia wachimbaji Arusha; zaidi ya watu 18 wanahofiwa kufariki.. Wanajeshi wafanaya uokozi sasa na tayari mtu mmoja ameokolewa hai na wengine watatu wakiwa wameshakufa!


KWA mujibu wa mashuhuda wa ajali iliyotokea leo asubuhi Jijini Arusha, inakadiriwa zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia kufukiwa na gema la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye malori.
Ajali hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje kidogo ya Jiji eneo jirani na Moshono-Kiserian ambapo vijana hao wanaokadiriwa kufikia idadi hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari mawili, moja ni Fuso na lingine kubwa zaidi (tani 18) na yote mawili yamefukiwa kabisa na kifusi.
Shuhuda mmoja wa ajali ambae pia ni mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa kawaida gari ndogo kama Fuso hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na watu 12 bila kuhesabu dereva na utingo.
Blog hii iliweza kushuhudia sehemu ndogo sana ya Fuso ikionekana lakini gari nyingine ilikua imefukiwa kabisa na kupondeka vibaya.
Miongoni wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa magari hayo. taarifa za eneo la tukio zinaeleza utingo mmoja ameokolewa akiwa amejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali lakini dereva wake amefariki dunia.
Katika eneo la ajali hali ni ya simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa kujizuia na kuangua kilio.
Meya wa Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana na kikosi cha Jeshi la Wananchi kufanya uokozi.
Blogu hii ilishuhudia pia Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator) kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na kifusi hicho.
ajali (66)Mwili wa dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa ndani ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram asubuhi ya leo
ajali (55)Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema asubuhi
ajali (44)Baadhi ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo halikupata nafasi
ajali (56)Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh Gaudence Lyimo akisaidiana na vikozi vya jeshi katika zoezi la uokozi
ajali (59)Mh Lema akiangalia namna vikosi vya Jeshi la Wananchi pamoja na askari Polisi wakiendelea na zoezi la uokozi
ajali (65)Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
ajali (49)Hali ilivyo machimboni hapo
ajali (64)Kina mama wakilia kwa uchungu wakihofu kuondokewa na wapendwa wao
ajali (21)Vikosi vya Jeshi la Wananchi na Polisi vikiwa kazini
ajali (35)Sehemu ndogo ya Fuso ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa
ajali (23)
ajali (2)Ambulance ya Jiji tayari tayari kwa lolote ikihitajika
ajali (3)
ajali (4)Wachina wakielekea eneo la jali na vifaa vyao kusaidia zaidi zoezi la uokozi
ajali (6)Wanajeshi zaidi wakielekea chini kwenye mgodi
ajali (21)
Tunaomba radhi kwa ubora hafifu wa picha hizi….

UPDATE ARUSHA: IDADI YA WALIOFARIKI DUNIA KWA KUFUKIWA NA KIFUSI IMEFIKIA 20




WATU zaidi ya 20 wamefariki dunia kwa kufukiwa na kifusi wakati wakichimba  mchanga aina ya Moramu katika machimbo  yaliyopo Moshono nje kidogo ya jiji la Arusha.


Tukio hilo ambalo limegubikwa na simanzi na vilio kwa ndugu jamaa na wananchi, limetokea leo majira ya saa 5 asubuhi wakati marehemu hao wakichimba na kupakia Moramu hiyo kwenye magari .


Pamoja na vifo hivyo magari mawili aina ya Fuso na Scania yameharibiwa vibaya baada ya kufukiwa na kifusi kilichoporomoka umbali unaofikia mita 50 kutoka usawa wa bahari.


Tayari kikosi cha uokoaji ambao ni  Jeshi la Wananchi Kambi ya Tanganyika Parkers kimefanikiwa kuopoa miili ya marehemu 16 waliofukiwa.


Baadhi ya miili ya marehemu  imetambulika kwa majina kuwa ni  Alex Maliaki, Gerald Hamis, Sauli Rafael (Mbu), Barick Loselian, Kababuu Lowasale, Mwenda Kibobori, Japhet Mjivaine na Garald Masai.


Taarifa za mashuhuda zimebainisha kwamba chanzo cha kuporomoka kwa kufusi hicho ni mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Arusha zilizosababisha kukatika kwa Ngema baada ya kuzidiwa na maji ya mvua.

ARUSHA:ZAIDI YA WATU 18 WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI KATIKA MACHIMBO YA MORRUM



Majeruhi aliyeokolewa.
Mwili wa mmojawapo wa marehemu.
Wananchi wa eneo hilo wakiwa na simanzi baada ya ajali hiyo.
----------
Watu zaidi ya 18 wanahofiwa kuwa wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi wakiwa ndani ya mgodi wa Morrum huko Moshono jijini Arusha. 

Kwa sasa wanajeshi wanaendelea na zoezi la uokoaji na tayari majeruhi mmoja ameokolewa na miili ya watu watatu. 

Tukio hili linatokea ikiwa ni siku siku tatu baada ya maafa mengine kutokea jijini Dar es Salaam ambapo watu zaidi ya 30 wamepoteza maisha baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka.