Nitaisambaratisha CCM Kanda ya Pwani-Mabere Marando

Makamu Mkiti wa Kanda ya Pwani wa Chadema Mabere Nyaucho Marando amesema kwamba ataisambaratisha CCM katika kanda hii.Huku akishangiliwa kwa mayowe na wajumbe na viongozi wa kanda hii inayojumuisha Dar es Salaam na Pwani,Marando amesema yeye amesomea ushushushu na atatumia Taaluma yake hiyo kuhakikisha CCM itabaki historia katika kanda hii.
Marando amesema atafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha anadhibiti mbinu zote za CCM.Na atatembea kila kona ya kanda hii kuizika CCM.
Viongozi wengine wa Kanda hii ni Mkiti Professor Abdallah Safari na Katibu wa Kanda Halima Mdee.
Marando ameongeza kwamba anaongoza kanda kubwa yenye watu wengi ambao idadi yao ni kama nchi ya Rwanda au Shelisheli.Hivyo ameahidi utumishi uliotukuka.

Posted by Chadema Blogtz at 11:15 PM