UPDATES FROM SOWETO ARUSHA

Askari Polisi kwa wingi wao, wakiwa na mabomu ya machozi, bunduki za risasi, maji ya kuwasha n.k, wamedamkia viwanja vya Soweto na kuweka zuio mtu yeyote asiingie ndani ya eneo hilo ambalo tayari kuna mahema na viti kwa ajili ya wanaChadema na watu wengine kuweza kushiriki tukio la kuaga marehemu waliokufa kwenye mlipuko wa bomu ambalo Mh Mbowe alitangaza jana kuwa mrushaji ni askari Polisi na watamtaja muda wowote wakimaliza kushauriana na wanasheria wa chama.
Kwa makadirio ya haraka mpaka sasa kuna watu kati ya 600 na 700 wameshatanda eneo hilo wakiwashangaa Polisi hao na zoezi linaloendelea wakidai hakuna kibali cha mkusanyiko eneo hilo. 

Haya ni maajabu mengine na ni sababu ya kuongeza tension kwa watu wenye majonzi... Kuna taarifa pia Askari wa JWTZ hawajapendezwa na hatua hiyo na wameshangaa ni kwanini watu wanazuiwa ilhali na viongozi wao wako hapo kuaga wapendwa wao. 

Ikumbukwe kwamba jana mtoto meingine ameongezeka kwenye idadi ya waliofariki na kuna watu kadaa wako ICU Arusha na Nairobi ambao sala zenu na dua zenu zitawaponya. 

Mmoja wa walioko ICU ya Selian Hospital ni pamoja na Meneja Kampeni wa Mgombea wa Chadema Kata ya Elerai ambae kwasasa hawezi kuongea tena. Anafahamika kama Bw Gabo. Gabo ana mtoto wa miaka miwili na marehemu Judy Mollel, Katibu wa Chadema Sokoni 1 na aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bawacha katika Kata hiyo..Judy alifariki papo hapo baada ya kulipiliwa na bomu akiwa na mwenza wake huyo ambao wote ni viongozi wa Chadema Arusha. 
Inatia simanzi na kuhuzunisha sana, na hasira pia (Mbowe aliwaambia maelfu ya wananchi jana walilipize kwa chochote zaidi ya sala kwa Mungu) hasa ukizingatia kuwa wahusika ni askari polisi na leo wanawazuia watu wasiage wapendwa wao!! So painful. 
Ushauri wangu, kama vipi hili Jeshi la Polisi na waliowatuma wazichukue maiti hizo wakazichemshe supu wanyewe ikiwa hawaguswi na chochoite katika hili. Ifahamike kuwa sio askari wote wakubwa kwa wadogo wamependezwa na yaliyaofanyika lakini kitendo cha kuweka vizuizi hivi kunawajumuisha wote na Jeshi zima. Kikubwa walipaswa kuonesha ushirikiano na kuongeza ulinzi kwa wale walio wema kwasababu hata jana Mbowe aliwataka wananchi kuacha hasira zao na wasiwazuie Polisi kufanya kazi zao. 


Ni hayo kwa sasa (picha iliyotumika ni ya mkusanyiko wa jana viwanja vya Soweto ambapo Mbowe alitoa taarifa zaidi kuhusiana na sakata hilo na kuweka bayana kuwa mhusika wamenfahamu kupitia rekodi za video viwanjani hapo) 

SeriaMtoto WikiLiks Tumainiel ON FB