Freemasons waivamia Moshi-Wabandika Matangazo ya Kujiunga Kila Kona




IMANI ya jamii ya siri ya Freemasons imeonekana kuuteka Mji wa Moshi na vitongoji vyake kutokana na matangazo mengi kubandikwa kila kona yakihamasisha wafuasi kujiunga huku ofa ya utajiri ikipewa kipaumbele.

Risasi Mchanganyiko limeshuhudia matangazo mengi yanayohamasisha kujiunga na imani hiyo yakiwa yamebandikwa kila kona ya mji huu ikiwemo katika nguzo za umeme


Katika tangazo hilo, wahusika wameeleza kwamba watakaojiunga mapema watapewa magari ya kifahari na nyumba za kisasa ikiwa ndiyo njia za awali za kubadilisha maisha yao.
Mwandishi wetu alijifanya anataka kujiunga na kupiga namba za simu zilizowekwa katika tangazo hilo ambazo ni 0783 127 967 ambapo ilipokelewa na mwanaume aliyekataa kutaja jina lake lakini alitoa masharti ya kujiunga.
“Tuma majina yako matatu; lako, baba na babu yako halafu tuma na shilingi 100,000 kwenye namba 0714 084 841 ambayo ni ada ya uanachama kisha utakwenda Kindoroko Hotel, chumba namba 87 hapo utakutana na bosi wangu na utaandikishwa rasmi na kupewa nguo zenye nembo yetu,” alisema mtu huyo.