JUKWAA LA WALIMU NA WANAFUNZI-TANZANIA LATOA TAMKO NA LAWAMA KWA MAPROFESA na MADOKTA(PhD) WA TANZANIA NDIO CHANZO CHA UBOVU WA ELIMU YA TANZANIA.


Kutokana na wanasiasa na wadau mbalimbali wa elimu kumsakama Waziri
Kawambwa na Baraza la mtihani la Taifa hii inatokana na 
Viongozi wetu
wa Tanzania kutokufanya tafiti ya kile wanachokisema. Tanzania tuna
Maprofesa na Madokta(PhD) wengi tu tena wengine wa siku nyingi lakini
hatuoni mchango wao katika kuboresha elimu ya Tanzania zaidi
wanaungana na wanasiasa kuendeleza porojo badala ya kutoa ufumbuzi wa
namna gani tutaiokoa elimu ya Tanzania.

Tulitegemea kuona Maprofesa na Madokta(PhD) kuibuka kwa nguvu kubwa
kuitaka serikali iunde mtaala wa elimu wenye tija kwa elimu ya
kitanzania na wao wakishiriki kutoa mchangoa wao badala yake ni
malumbano yasiyokuwa na tija. Hata tume inayotazamiwa kuundwa na
waziri mkuu tulitegemea Maprofesa wangekuwa wa kwanza kutoa ufumbuzi
kabla hata tume haijaanza kazi. Tunajua Maprofesa na Madokta(PhD)
wanauwezo mzuri wa kuandika mtaala wa elimu na sera nzuri ya elimu
hata kutunga Vitabu vizuri vya kufundishia kutokana na kiwango chao
cha elimu lakini tumewaachia Kina Nyambari watunge vitabu na watu wake
wakati tuna wasomi wa ngazi ya juu kabisa, tusiwe Taifa la kulaumu
bali tuwe Taifa la kujenga na kuona uchungu wa watoto wetu.

Hata kama tume ya waziri mkuu itapita bado suluhu haitapatikana
kutokana na wanao jua ukweli wamekaa kimya au kuamua kufanya kazi ya
siasa. Sambamba na mitaala na mfumo mbovu wa elimu wa nchi yetu bado
serikali inatakiwa kujitahimini juu ya mishara ya walimu kwani ni
midogo sana na haiendani kabisa na mazingira wanayoishi. Mwalimu
mwenye degree analipwa takribani 500,000/= na usheee, diploma
takribani 300,000/= na ushee na mwenyecheti takribani 200,000/= na
ushee unategemea nini hapo?



Kimsingi mishara ni midogo sana na kila siku kodi za nyumba zinapanda
vyakula vinapanda, umeme unapanda kila mara nauli za daladala, kweli
mtu una weza kuishi? Huo huo mshahara ukatwe kodi ,ukatwe Nssf ,
ukatwe CWT, chama cha kutetea haki za wafanya kazi wachukue chao.
1.Nauli kwa siku 800 kwa siku sita ni Tsh ngapi?
2.kodi ya chumba kwa mwezi 30,000/=
3.Chai asubuhi 800/=
4.chakula mchana 1200/=
5.kodi ya umeme 10,000/=
6.maji ya kununua ya madumu 300/=
7.Nyumbani uache 3500/=
8.Mtoto apate nauli ya shule na kula kwasiku 2000/=
9.Bado matumizi ya matibabu japo hili linatokea mara chache
Tunaomba mlitazame .

Lakini hutasikia wabunge na wanasiasa wanapiga kelele kutetea mishara
ya walimu ila wao kujiongezea posho wanajipigia kelele sana na
wanaishi maisha ya kifahari kuliko sisi walimu. Tulitegemea wabunge
wange wasilisha hoja binafsi ya kutetea mishahara ya watumishi ili
wafanye kazi kwa moyo wote lakini utafikiri hawaoni, daima tunajua
mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa. Mwalimu hata angejituma
vipi kama mshahara haukidhi ni vigumu kufundisha kwa kujituma maana
lazima awaze kufanya biasahara nje ya kazi ukizingatia mwalimu hana
hata motisha.

Matokeo ya kidato cha nne yawe changamoto kwa serikali na si kutafuta
mchawi bali mchawi mkubwa ni mshahara mdogo na walimu kuthaminiwa.

Mwl.DEOGRATIUS KISANDU
Mwenyekiti wa JUKWAA LA WALIMU NA WANAFUNZI-TANZANIA.
25/02/2015