Taswira: Mh Mbowe Ashuhudia Makabidhiano Rasmi ya Eneo Lenye Thamani ya Shilingi Mil 480 Baina ya Mbunge wa Arusha Mjini na Kampuni ya Mawalla Advocates Kwa Ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto Jijini Arusha Leo



DSCN7646
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh Freeman Mbowe, ambe pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni akihutubia katika hafla ya makabidhiano ya kiwanja alichoahidiwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema na Kampuni ya Mawalla Advocates na Mawalla Trust ya Jijini Arusha leo asubuhi.
Hafla hiyo fupi ilifanyika katika kiwanja hicho chenye ukubwa wa ekari tatu eneo la Burka, nje kidogo ya Jiji. Kiwanja hicho kinathamani ya Jumla ya shilingi milioni 480 (USD 300,000).
Mbowe alisifu jitihada za Mbunge Lema kupigania maendelo ya watanzania, na pia akakumbushia ulazima wa nafasi tano za madiwani kuzibwa mapema iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa ArDF (Mfuko wa Mbunge Lema kwa Maendeleo ya Arusha),Bw Elifuraa alisema mradi huo wa hospitali ya mama na mtoto utasimamiwa kwa karibu na taasisi hiyo lakini haitakuwa jukumu lake pekee bali wananchi wote bila kujali itikadi zao.
Elifuraa alisema tayari mchora ramani amekwishapatikana na kupatiwa jukumu la kuandaa michoro lakini pia ArDF wanafanya mawasiliano na madaktari bingwa ili waweze kutoa mawazo yao ili jengo liwe la kisasa zaidi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema alisema kwamba tukio hili la leo ni faraja sana kwake na ni jibu kwa wote walioandika ama kuzungumza mabaya dhidi yake siku za nyumba kwamba alishakabidhiwa viwanja hivyo na kuviuza, kitu amcho amedai leo imedhihirika ukweli na uongo ni upi.
Lema ameahidi kutimiza kila ahadi aliyowaahidi watanzania hususani wakazi wa Arusha na kwa kuazna na hospitiali ya kina mama na watoto amedai mipango iliyopo ni mpaka kufikia mwezi Juni mwaka huu jengo la Utawala la hospitali hiyo litakuwa tayari.

DSCN7652Mh Mbowe na baadhi ya viongozi wa Chadema, Wawakilishi wa Mawala Advocates, Madiwani wa Chadema, Waandishi wa Habari na wananchi wakikagua mipaka ya shamba hilo
DSCN7649
DSCN7633Baadhi ya waandishi wa habari na mabloga wakiwa kazini
DSCN7639Mkurugenzi wa Mawala Trust, Bw Godfrey Mawalla akimkabidhi Mh Lema hati za viwanja hivyo vyenye thamani ya shilingi miliono 480. Ilielezwa kuwa lengo la matumizi ya viwanja hivyo ni kwa ujenzi wa hopsitali hiyo ya kuhudumia kina mama na watoto na si vinginenvyo.
DSCN7635Mwakilishi mwingine wa kampuni ya Mawalla Advocates na Mawalla Trust akitoa salamu
DSCN7620Mh Mbowe akiwasili shambani hapo
DSCN7628Mratibu wa maswala ya wanawake Chadema Arusha, Bi Cecilia Ndosi akizungumza katika hafla hiyo, akiwakilisha kina mama ambao ndio walengwa wakubwa wa mradi huo, bila kusahau watoto wao.
DSCN7627Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA Jijini Arusha, akitoa neno kwa niaba ya madiwani wenzake
DSCN7630Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendelo Arusha (ArDF), Bw Elifuraha akitoa ufafanuzi kuhusiana na mradi wa hopsitali ya mama na mtoto inayotarajiwa kujengwa eneo la Burka chini ya usimamizi wa taasisi hiyo
DSCN7632
DSCN7611Baadhi ya waandishi wa habari wakiingia eneo la shughuli rasmi ya makabidhiano hii leo