VITUO VIWILI VYA REDIO VYAFUNGIWA,KIMOJA CHAPEWA ONYO KALI NA FAINI




Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maadili ya Utangazaji nchini, Walter Bgoya (katikati) akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam ukumbi wa habari Maelezo

Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo
KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.
Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.
Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.
Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa kufanya.


Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa wakiviamini vituo hivyo.
Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.

VINARA TISA URAIS 2015


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod
WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.
Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.

Katika matokeo ya utafiti huo uliofanywa Desemba mwaka jana, Dk Slaa anafuatiwa kwa mbali na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amefungana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kila mmoja akipata asilimia tisa.

Hata hivyo, licha ya kuongoza, Dk Slaa ameporomoka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na matokeo ya utafiti kama huo uliofanywa na taasisi hiyo mwaka 2011 ambapo alipata asilimia 42.

Kadhalika, umaarufu wa Pinda ambaye anaongoza miongoni mwa wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeshuka kwa asilimia tatu kutoka 12 za mwaka juzi, wakati Zitto ameendelea na kiwango kilekile cha asilimia tisa alizopata katika utafiti uliotangulia.
Wengine wanaofuata na asilimia walizopata kwenye mabano ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (8), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (7) na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (5).

Pia wamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (4) ambaye amefungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (4) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta (2).
Ikilinganishwa na utafiti wa 2011, Lipumba ameporomoka kwa asilimia tisa.
Lowassa amepanda kwa asilimia sita, Dk Magufuli asilimia nne, Mbowe na Membe wamepanda kwa asilimia mbili kila mmoja, wakati Sitta amebaki katika kiwango kilekile cha asilimia mbili.

Hata hivyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi ambao hawana uamuzi wa kuchagua mtu yeyote kati
ya hao kwa sasa ni asilimia 18, likiwa ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na utafiti uliotangulia.

CCM yatamba
Katika utafiti huo, CCM kimeonyesha kuwa ni chama ambacho asilimia 52 ya wananchi wangependa kujiunga nacho, kikiwa kimepanda chati kwa asilimia moja kutoka asilimia 51 mwaka jana.

Kwa upande wa Chadema, wananchi ambao wanapenda kujiunga nacho imeshuka kutoka asilimia 35 mwaka 2011 hadi 31 mwaka jana.

Uwezekano mkubwa wa CCM kupanda chati ni kutokana na ukweli kuwa mwaka jana kilikuwa na uchaguzi ulioanzia ngazi ya mashina hadi taifa na kuibua vuguvugu kubwa masikioni mwa wananchi.

Chadema hakikuwa na harakati kubwa za kisiasa ukiacha kampeni ya Movement For Change (M4C), ambayo kwa kiasi haikuwa na pilika kama uchaguzi wa CCM.
Chama kingine ni CUF ambacho kimeporomoka kwa kupata asilimia 10 mwaka 2011 hadi nne mwaka 2012.

Hata hivyo, asilimia ya wananchi kutokutaka kujihusisha na chama chochote imepanda kutoka asilimia mbili mwaka 2011 hadi 12 mwaka 2012.

Rushwa
Katika suala la rushwa nchini, utafiti huo umeonyesha kuwa kati ya watu 10 waliohojiwa, wanne walikuwa na maoni kuwa rushwa imeongezeka kufikia asilimia 41, asilimia 30 walisema iko palepale, asilimia 23 walisema imepungua na asilimia tano hawajui.Utafiti huo unaonyesha kuwa mapambano dhidi ya rushwa hayajabadilika tangu 2011katika taasisi za Serikali ukisema haionekani kama kuna utashi wa kisiasa kupambana na tatizo hilo katika taasisi hizo kama Jeshi la Polisi na Mahakama ambazo zimeonekana kuwa nyuma katika mapambano hayo.

Katika utafiti huo, polisi ndiyo inayoongoza kwa rushwa baada ya asilimia 33 ya watu waliohojiwa kulitaja jeshi hilo, ikifuatiwa na Mahakama asilimia 16 na sekta ya afya ikiwa na asilimia 16.

Utafiti huo umeonyesha matatizo makubwa yanayoikabili nchi kwa sasa ni njaa, gharama za maisha, umaskini, migogoro ya kidini na ukosefu wa ajira.

“Asilimia 50 wametoa maoni kuwa njaa ni tatizo kubwa ikifuatiwa na gharama za maisha asilimia 44, migogoro ya ya kidini asilimia 43 na ukosefu wa ajira asilimia 34.”

“Inamaanisha kuwa rushwa na mfumuko wa bei havichukuliwi kama ni tatizo kwa Watanzania wengi kama ilivyojionyesha mwaka 2011,” inaeleza taarifa ya utafiti huo.
Wananchi wameeleza kuwa mambo muhimu ambayo yanatakiwa kupewa kipaumbele ni pamoja na sekta ya afya kwa asilimia 24, elimu asilimia 21, ajira asilimia 18, chakula asilimia 17 na miundombinu asilimia 16.

TUME YA PINDA KIINI MACHO TU:




KAMA ilivyotarajiwa, wananchi wengi wamebeza hatua ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kuunda tume ya kuchunguza matukio mabaya ya kidato cha nne kwa mwaka 2012. Pamoja na kuona hatua hiyo ya Waziri Mkuu kama kiinimacho tu, wamesema haitakuja na jambo jipya kwa kuwa huko nyuma tume za aina hiyo ziliundwa siyo kwa lengo la kutatua matatizo, bali kwa kufunika kombe ili mwanaharamu apite.

Kwa maana hiyo, Serikali imekuwa ikiunda tume nyingi ikiwa kama njia ya kupata muda wa kupumua baada ya kutokea matukio mabaya kama hilo la mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka jana na kutangazwa wiki iliyopita.
Kama ilivyotokea katika tukio hilo la wiki iliyopita, wananchi wamekuwa wakikasirishwa na kughadhabishwa na matukio ambayo wanaona yanasababishwa na Serikali na madhara yake kuwa mwiba mkali kwa wananchi.

Hata baada ya kuunda tume hizo, Serikali imekuwa haiyafanyii kazi mapendekezo yaliyomo katika ripoti za tume hizo. Mara nyingi Serikali imekuwa ikizikalia ripoti hizo na kuzifanya siri. Wakati mwingine imekuwa ikitangaza baadhi ya vipengele inavyoona havielekezi lawama kwa Serikali moja kwa moja au kuwa na nguvu zinazoweza kuchochea hasira kali za wananchi dhidi yake, hivyo kuilazimisha kuwajibika.

Ndiyo maana wengi wanadhani Tume ya Pinda ni kiinimacho tu na kwamba hapakuwapo sababu ya kuunda chombo hicho kitakachofuja fedha za walipa kodi wakati matatizo yaliyosababisha matokeo hayo ya aibu katika mtihani huo yako wazi kama ilivyo usiku na mchana.

Moja ya sababu zinazowafanya wananchi wakose imani na tume hiyo ni hatua ya Serikali ya kukataa kuwaweka kando viongozi wakuu wa wizara husika ili wapishe uchunguzi na kuiwezesha tume hiyo kutoa matokeo ya uhakika bila kuingiliwa na upande wowote kwa lengo la kuinusuru sekta ya elimu.

Wananchi wanazo sababu za msingi kwa kutokuwa na imani na tume zinazoundwa na Serikali. Mwaka 2004 aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye aliunda tume kuangalia matatizo katika sekta ya elimu. Tume nyingine iliundwa mwaka 2010.

Tume ya mwaka 2011 ilihusu Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa lengo la kuchunguza sababu za walimu kufeli katika vyuo vya ualimu. Tume hizo zilitoa ripoti, lakini Serikali haijawahi kutangaza matokeo au kuwaeleza wananchi juu ya hatua zilizochukuliwa.

Kwa jambo zito kama hilo la anguko la kihistoria katika mtihani wa kidato cha nne, wengi walitegemea kwamba Rais Jakaya Kikwete kwanza angetangaza hali hiyo kama janga la kitaifa.

Hiyo ingefuatiwa kwa karibu na kuunda tume ya kuchunguza tukio hilo na kuwaweka kando viongozi wakuu wa wizara husika, akiwamo Waziri Shukuru Kawambwa ili kupisha uchunguzi.
Lakini tunachoshuhudia hivi sasa ni mwendelezo wa utamaduni wa kulindana, licha ya ukweli kwamba kiwango cha elimu kimekuwa kikiporomoka mwaka hadi mwaka chini ya uongozi wa Waziri Kawambwa.

Hakuna asiyejua kwamba mfumo wa elimu katika nchi yetu ulikufa miaka mingi iliyopita na haikuwa rahisi kuufufua kutokana na wanasiasa kufanya elimu kuwa suala la kisiasa. Ujenzi wa shule za kata, kwa mfano lilikuwa jambo la kheri, ingawa ulifanyika kwa kukurupuka ili kutimiza malengo ya kisiasa ya chama fulani.

Ni matumaini yetu kwamba Tume ya Pinda haitafanya kazi kisiasa, bali itatoa majibu hadharani jinsi ya kuusuka upya mfumo wetu wa elimu ambao umevurugika.

JUKWAA LA WALIMU NA WANAFUNZI-TANZANIA LATOA TAMKO NA LAWAMA KWA MAPROFESA na MADOKTA(PhD) WA TANZANIA NDIO CHANZO CHA UBOVU WA ELIMU YA TANZANIA.


Kutokana na wanasiasa na wadau mbalimbali wa elimu kumsakama Waziri
Kawambwa na Baraza la mtihani la Taifa hii inatokana na 
Viongozi wetu
wa Tanzania kutokufanya tafiti ya kile wanachokisema. Tanzania tuna
Maprofesa na Madokta(PhD) wengi tu tena wengine wa siku nyingi lakini
hatuoni mchango wao katika kuboresha elimu ya Tanzania zaidi
wanaungana na wanasiasa kuendeleza porojo badala ya kutoa ufumbuzi wa
namna gani tutaiokoa elimu ya Tanzania.

Tulitegemea kuona Maprofesa na Madokta(PhD) kuibuka kwa nguvu kubwa
kuitaka serikali iunde mtaala wa elimu wenye tija kwa elimu ya
kitanzania na wao wakishiriki kutoa mchangoa wao badala yake ni
malumbano yasiyokuwa na tija. Hata tume inayotazamiwa kuundwa na
waziri mkuu tulitegemea Maprofesa wangekuwa wa kwanza kutoa ufumbuzi
kabla hata tume haijaanza kazi. Tunajua Maprofesa na Madokta(PhD)
wanauwezo mzuri wa kuandika mtaala wa elimu na sera nzuri ya elimu
hata kutunga Vitabu vizuri vya kufundishia kutokana na kiwango chao
cha elimu lakini tumewaachia Kina Nyambari watunge vitabu na watu wake
wakati tuna wasomi wa ngazi ya juu kabisa, tusiwe Taifa la kulaumu
bali tuwe Taifa la kujenga na kuona uchungu wa watoto wetu.

Hata kama tume ya waziri mkuu itapita bado suluhu haitapatikana
kutokana na wanao jua ukweli wamekaa kimya au kuamua kufanya kazi ya
siasa. Sambamba na mitaala na mfumo mbovu wa elimu wa nchi yetu bado
serikali inatakiwa kujitahimini juu ya mishara ya walimu kwani ni
midogo sana na haiendani kabisa na mazingira wanayoishi. Mwalimu
mwenye degree analipwa takribani 500,000/= na usheee, diploma
takribani 300,000/= na ushee na mwenyecheti takribani 200,000/= na
ushee unategemea nini hapo?



Kimsingi mishara ni midogo sana na kila siku kodi za nyumba zinapanda
vyakula vinapanda, umeme unapanda kila mara nauli za daladala, kweli
mtu una weza kuishi? Huo huo mshahara ukatwe kodi ,ukatwe Nssf ,
ukatwe CWT, chama cha kutetea haki za wafanya kazi wachukue chao.
1.Nauli kwa siku 800 kwa siku sita ni Tsh ngapi?
2.kodi ya chumba kwa mwezi 30,000/=
3.Chai asubuhi 800/=
4.chakula mchana 1200/=
5.kodi ya umeme 10,000/=
6.maji ya kununua ya madumu 300/=
7.Nyumbani uache 3500/=
8.Mtoto apate nauli ya shule na kula kwasiku 2000/=
9.Bado matumizi ya matibabu japo hili linatokea mara chache
Tunaomba mlitazame .

Lakini hutasikia wabunge na wanasiasa wanapiga kelele kutetea mishara
ya walimu ila wao kujiongezea posho wanajipigia kelele sana na
wanaishi maisha ya kifahari kuliko sisi walimu. Tulitegemea wabunge
wange wasilisha hoja binafsi ya kutetea mishahara ya watumishi ili
wafanye kazi kwa moyo wote lakini utafikiri hawaoni, daima tunajua
mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa. Mwalimu hata angejituma
vipi kama mshahara haukidhi ni vigumu kufundisha kwa kujituma maana
lazima awaze kufanya biasahara nje ya kazi ukizingatia mwalimu hana
hata motisha.

Matokeo ya kidato cha nne yawe changamoto kwa serikali na si kutafuta
mchawi bali mchawi mkubwa ni mshahara mdogo na walimu kuthaminiwa.

Mwl.DEOGRATIUS KISANDU
Mwenyekiti wa JUKWAA LA WALIMU NA WANAFUNZI-TANZANIA.
25/02/2015

MWANAMUZIKI WA BONGO FLAVA AL MAARUFU KWA JINA LA ''TIMBULO''''' AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA HUKO BURUNDI.





Msanii wakizazi kipya, anae ondoka na mitindo ya bongo flava Ally TIMBULO kuna tetesi zinasema kuwa amekamatwa na dawa zakulevya Mjini Bujumbura .......


Habari zinadai kwamba Msanii huyo alikuwa na mpango waku endesha tamasha Mjini Bujumbura mwezi wa 4 baada ya maombi lukuki ya washabiki wake Mjini Bujumbura/nchini Burundi . ......



Mtandao huu unaendelea kufuatilia undani wa tukio hili

STIVE NYERERE "ATIWA RUMANDE" ASUBUHI HII BAADA YA KUVAANA KWA MANENO NA POLISI




Eneo la tukio la ajali hiyo.
Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.
Kushoto ni gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari lililohusika na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.

Askari wa usalama barabarani, akipima ajali hiyo.
Askari akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka kituoni Mabatini.
Gari la Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari jingine.
Gari husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.
Baadhi ya warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa washiriki wa Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio.
Movie mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive Nyerere, iliyokuwa ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi hii.
Msanii huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo cha Mabatini, wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki katika Movie hoyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.
Wasanii hao pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao iliyokuwa maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na kufanyia mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.
Ajali hiyo ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo.
Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni. 
Mashuhuda wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, ili kuepusha madhara zaidi.
Baada ya ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.
Katika majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo kulitokea kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo, aliyediriki kumuita Stive mjinga, ambapo Stive alishindwa kuvumilia na kuamua kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi katika gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye kuelekea katika Kituo cha Mabatini. 
credits: Sufiani Mafoto

MIJI YENYE GHARAMA ZAIDI DUNIA


LONDON, Uingereza
MIJI ya Sydney na Melbourne ni miongoni mwa maeneo yanayotajwa kuwa na gharama kubwa zaidi za maisha duniani.
Miji hiyo ambayo iko nchini Australia, imeingia katika nafasi ya tano bora.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kitengo cha Kiintelijensia cha Uchumi Duniani (EIU), gharama za maisha katika miji hiyo imezidi hata miji ya Ulaya na Marekani.
Bara la Asia na Australia lina miji 11 kati ya 20 iliyotajwa kuwa na gharama za juu za maisha duniani, huku miji minane ikitoka Ulaya na mmoja ukitoka America ya Kusini.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kitengo hicho, licha ya bara la Amerika ya Kaskazini kuwa na nchi maarufu na zenye uchumi wa juu, hakuna hata mji mmoja ulioweza kuingia kwenye 20 bora.
Katika utafiti uliofanyika miaka 10 iliyopita kulikuwako na  miji sita kutoka barani Asia, 10 kutoka Ulaya na minne kutoka Marekani katika 20 bora kwenye orodha ya miji 131 yenye gharama za juu kwenye nchi 93 duniani.
Katika utafiti  uliotolewa mwaka huu, Jiji la Tokyo limeshika nafasi ya kwanza likiliweka pembeni Jiji la Zurich ambalo lilikuwa kwenye nafasi hiyo na kuporomoka hadi kufikia nafasi ya saba.
Hii ni kutokana na sera za udhibiti wa mapato ya ndani ya nchi ya Uswiz kushuka.
Mji wa Osaka nchini Japan unashikilia nafasi ya pili katika orodha hiyo.
Jon Copestake, mhariri wa jarida la EIU alisema moja kati ya mabadiliko yaliyojitokeza ilikuwa ni kupanda kwa gharama nchini Australia, kulikouweka Mji wa Sydney kushika nafasi ya tatu huku Melbourne ikishika nafasi ya tano. Mji wa Oslo wa Norway ukishika nafasi ya nne. “Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, miji ya Australia haikuweza kuingia hata kwenye hamsini bora. Sijawahi kuona upandaji huu wa ghafla,” Copestake aliliambia Reuters.
“Lakini hii inatokana na kukua kwa uchumi kunakoendana na mfumuko wa bei pamoja na  kuimarika kwa Dola ya Australia dhidi ya Dola ya Marekani. Wageni wanaofika hapo huona kuna tofauti kubwa ya kimaisha huku wenyeji wakizoea maisha ya juu.
Kupanda kwa gharama barani Asia
Utafiti huo ulifanyika kwa kuangalia gharama za zaidi ya bidhaa 160 ukilenga kwenye vyakula, mavazi, huduma za nyumbani, usafiri na vitu vidogovidogo.
Copestake haikushangaza sana kwa Mji wa Tokyo kurejea kwenye miji ya inayoongoza, hii ni kutokana na kukua kwa uchumi wa Japan jambo linalosababisha kuongezeka kwa gharama za mahitaji muhimu kama vile mapango ya nyumba, mishahara na hata bei za nishati ya mafuta.
Tangu mwaka 1992 Tokyo imekuwa kwenye sita bora huku miji ya  Zurich, Paris na Oslo ikidaiwa kushika nafasi ya kwanza.
Miji mingine iliyoingia kwenye 10 bora kwa mwaka 2013 ni

Singapore, Zurich, Paris,Caracas na Geneva.
Akizungumzia kuhusu nchi za Ulaya, Copestake alisema woga wa kushuka kwa uchumi wao na kuimarika kwa Euro kumechangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa gharama za maisha kwa miji ya bara hilo, huku kwa Mji wa Carcas kumetokana na kukua kwa udhibiti wa viwango vya ubadilishaji wa fedha.
Licha ya kutokuwako kwa miji ya Amerika ya Kaskazini kwenye 20 bora, EIU imesema gharama za maisha kwa mji wa Washington  zilikuwa zikiongezeka ukilinganisha na maeneo mengine ya Marekani. Mji huo umeshika nafasi ya 27 ukifungana na Mji wa Los Angeles.
Mji wa Vancouver wa nchini Canada umeendelea kushika nafasi ya 21, ukiwa ni mji wenye gharama za juu zaidi za maisha kwa nchi za Amerika ya Kaskazini.
Hata hivyo, wakati Bara la Asia na  Australia kuna jumla ya miji 11 iliyoingia kwenye 20 bora, inasemekana ni eneo ambalo lina miji sita kati ya 10 yenye gharama rahisi zaidi duniani.
Mji wa Mumbai kutoka nchini India na Karachi wa Pakistan ni miongoni mwa miji iliyotajwa kuwa na gharama za chini za maisha katika utafiti huo ikifuatiwa na New Delhi, Kathmandu na Algiers.
Nchi ya India imekuwa na tofauti kubwa kimaisha kwa baadhi ya miji kutokana na kuwepo kwa tofauti ya mgawanyo wa miundombinu.
Hii ndiyo sababu kubwa ya kuweko kwa miji yenye gharama za juu zaidi na ile yenye gharama za chini zaidi.
Miji mingine iliyoshika nafasi kumi za mwisho katika utafiti huo ni pamoja na Bucharest wa Romania, Colombo wa Sri Lanka, Panama City, Jeddah wa Saudi Arabia, na Teheran wa Iran.

Catholic priest, Padre Evarist Mushi shot to death in Zanzibar on his way to church


padre-evarist-mushiCatholic priest, Padre Evarist Mushi of Minara Miwili Catholic church’s parish in Mtoni, Zanzibar was shot and killed by unidentified gunment who were on a Vespa motorcycle.



According to millardayo.com, the asailant fired a single bullet into father Mushi’s head and fled the scene on their motorcycle.
“Father Evarist Mushi was blocked by two young men at the entrance of the church, one of the attackers shot him in the head,” said the island’s police spokesman Mohammed Mhina.
This is a second attack on a Catholic priest in semi-autonomous Zanzibar archipelago in the past few months. On Christmas Day, gunmen shot and seriously wounded a Catholic priest as he returned home from church.
It is not clear if the two attacks were linked, or religiously motivated.
Father Mushi was shot as he was stepping outside of his car on his way to the church to lead Sunday’s service.

Story framed by http://live.com

Freemasons waivamia Moshi-Wabandika Matangazo ya Kujiunga Kila Kona




IMANI ya jamii ya siri ya Freemasons imeonekana kuuteka Mji wa Moshi na vitongoji vyake kutokana na matangazo mengi kubandikwa kila kona yakihamasisha wafuasi kujiunga huku ofa ya utajiri ikipewa kipaumbele.

Risasi Mchanganyiko limeshuhudia matangazo mengi yanayohamasisha kujiunga na imani hiyo yakiwa yamebandikwa kila kona ya mji huu ikiwemo katika nguzo za umeme


Katika tangazo hilo, wahusika wameeleza kwamba watakaojiunga mapema watapewa magari ya kifahari na nyumba za kisasa ikiwa ndiyo njia za awali za kubadilisha maisha yao.
Mwandishi wetu alijifanya anataka kujiunga na kupiga namba za simu zilizowekwa katika tangazo hilo ambazo ni 0783 127 967 ambapo ilipokelewa na mwanaume aliyekataa kutaja jina lake lakini alitoa masharti ya kujiunga.
“Tuma majina yako matatu; lako, baba na babu yako halafu tuma na shilingi 100,000 kwenye namba 0714 084 841 ambayo ni ada ya uanachama kisha utakwenda Kindoroko Hotel, chumba namba 87 hapo utakutana na bosi wangu na utaandikishwa rasmi na kupewa nguo zenye nembo yetu,” alisema mtu huyo.

CLUBU MPYA YA KISASA YAFUNGULIWA ARUSHA


Huu ni muonekano wa jengo la world garden inavyoonekana kwa nje
 Hapa ni geti kuu la kuingialia katika jengo la world garden ilipo mushono ndani ya jiji la Arusha
 Katikati mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa mulongo akiwasili kuzindua rasmi jengo hili la world garden
wadau mbalimbali walishiriki katika uzinduzi wa ukumbi huu wa world garden ambapo katika jengo hili kuna vitu mbalimbali ikiwemo ukumbi wa disco afrika mashariki na kati hakuna kama huu kwani ni mkubwa na pia ni mzuri kuliko yote
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akizindua jiwe la msingi katika jengo hilo
 Mkuu wa mkoa wa Arusha akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wakiwa wanakata utepe wa lango kuu la kuingialia katika jengo hilo
 Mkuu wa mkoa wa Arusha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya World Garden wakiwa wanatembelea jengo hilo mbara baada ya mkuu huyo kuzindua rasmi apa ni ngazi za kuingilia katika ukumbi wa disco
mkuu wa mkoa akiwa na vingozi wengine pamoja na wageni waalikwa wakiangalia jinsi jengo hilo lilivyo ndani hapa wapo ndani ya ukumbi wa disco
Mkuu wa Mkoa akiteta jambo na Mkurugenzi mtendaji wa World Garden




 picha juu na chini maeneo mbalimbali ya ukumbi huo ikiwemo sehemu za kupumzikia ukiwa disco au klabu
hii ni kaunta ilikuwa bado aijawekwa vinjwaji lakini ndo muonekano wake huo
Hapa ndipo ma-dj wanakaa kufanya mambo
huu ni ukumbi wa mikutano uliopo ndani ya jengo hilo la world garden usipime na usiache kutembelea kwa kesho ambapo ni siku ya wapendanao kutakuwa na disco zuri kutaka kwa madj wakali ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu 15 tu
******************* 
MKUU wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha kuanza kuwekeza katika sekta mbalimbali ili kuweza kuweka mkoa wetu katika madhari  na hadhi ya jiji
Aliyasema hayo jana wakati akifungua jengo jipya la mikutano pamoja na ukumbi wa disco lililopo jijini hapa lijulikanalo kwa jina la World garden lililopo katika kata ya mshono ndani ya jiji la Arusha
Alisema kuwa   mkoa wa arusha kwa sasa umepandishwa hadhi na kuwa jiji hivyo ni wajibu wa wazawa kuwekeza katika mambo mbalimbali  akitolea mfano kuwa mpaka sasa pamoja ya kuwa   wananchi ni wengi na wageni ni wengi lakini mpaka sasa kuna sehemu super makerti moja tu kitu ambacho kinatia aibu kwa jiji kubwa kama hili
Alisema kuwa viwanja vipo vya kujengea sehemu hizo ni watu wa kuwekeza tu hivyo aliwasihi wawekezaji wajitokeze kwa wingi kuwekeza katika vitu mbalimbali ili kuweza kuwezesha jiji letu kuwa la kimataifa
Alibainisha kuwa wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wanaogopa kwenda kuchukumikopo na kuwekeza katika vitu mbalimbali lakini aliwatoa hofu na kuwaambia kuwa mikopo ipo na ni haki ya kila mmoja kwenda kuchukuwa mkopo kwani nafasi zipo wazi na mikopo ipo ya kutosha huku akibainisha kuwa amna mfanyabishara yeyote mkubwa anafanya kitu pasipo kuchukuwa mkopo
Alipongeza uongozi wa kampuni ya world garden na kudai kuwa wameweza kupiga atua kubwa kwani kufungua kwao kwa jengo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa kwani vijana wengi watapata ajira kupitia jengo hilo kwani katika jengo hilo kuna vitu vingi kwama vile ukumbi wa disco watu wa usafi wa nje na mengine mengi ambapo watu wote wanaotakiw akufanya kazi huku  ni watanzania vijana hivyo watakuwa wamesaidia vijana kupata ajira
Kwa upande wake  mkurugenzi mtendaji wa World garden alisema kuwa wao kama kampuni yao inampango wa kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 120 na pia alisema kuwa watajitaidi kuboresha vitu mbalimbali
PICHA NA WOINDE SHIZZA WA LIBENEKE LA KASAKAZINI BLOG

UMESHAISOMA BARUA ALIYOANDIKA DAKTARI KWA FAMILIA YA MAREHEMU ILIYOSOMWA NA ZAIDI YA WATU MILIONI 2 SAIVI DUNIANI??????

An emergency room doctor at New York Presbyterian Hospital has touched the hearts of millions after a personal letter he wrote about the death of a patient went viral on the Internet.

The letter was first published on Reddit by the son of the deceased woman, who reportedly died ofbreast cancer in December 2012. In the letter, the doctor explains that this is the first such note he has written in 20 years of ER work.

The letter has already been viewed by more than 2 million users on Reddit, with thousands leaving comments. The doctor's letter:

Dear Mr. (removed),

I am the Emergency Medicine physician who treated your wife Mrs (removed) last Sunday in the Emergency Department at (hospital). I learned only yesterday about her passing away and wanted to write to you to express my sadness. In my twenty years as a doctor in the Emergency Room, I have never written to a patient or a family member, as our encounters are typically hurried and do not always allow for more personal interaction.

However, in your case, I felt a special connection to your wife (removed), who was so engaging and cheerful in spite of her illness and trouble breathing. I was also touched by the fact that you seemed to be a very loving couple. You were highly supportive of her, asking the right questions with calm, care and concern. From my experience as a physician, I find that the love and support of a spouse or a family member is the most soothing gift, bringing peace and serenity to those critically ill.

I am sorry for your loss and I hope you can find comfort in the memory of your wife’s great spirit and of your loving bond. My heartfelt condolences go out to you and your family.

(removed), MD


The 24-year-old man who posted the letter said in an email interview with the Huffington Post that the outpouring of support from Reddit users has helped him cope with the passing of his mother.

"If my mother were alive to see this, she would want readers to reflect on the power of showing compassion toward a total stranger," he said in the interview. "The support I got from Reddit was amazing—doctors, nurses and other Redditors who have lost their mothers to cancer were all shocked and amazed that the doctor took the time to write such a heartfelt, meaningful letter.”

ISOME ZAIDI HAPA     na  HAPA

Taswira: Mh Mbowe Ashuhudia Makabidhiano Rasmi ya Eneo Lenye Thamani ya Shilingi Mil 480 Baina ya Mbunge wa Arusha Mjini na Kampuni ya Mawalla Advocates Kwa Ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Mama na Mtoto Jijini Arusha Leo



DSCN7646
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mh Freeman Mbowe, ambe pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni akihutubia katika hafla ya makabidhiano ya kiwanja alichoahidiwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema na Kampuni ya Mawalla Advocates na Mawalla Trust ya Jijini Arusha leo asubuhi.
Hafla hiyo fupi ilifanyika katika kiwanja hicho chenye ukubwa wa ekari tatu eneo la Burka, nje kidogo ya Jiji. Kiwanja hicho kinathamani ya Jumla ya shilingi milioni 480 (USD 300,000).
Mbowe alisifu jitihada za Mbunge Lema kupigania maendelo ya watanzania, na pia akakumbushia ulazima wa nafasi tano za madiwani kuzibwa mapema iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti wa ArDF (Mfuko wa Mbunge Lema kwa Maendeleo ya Arusha),Bw Elifuraa alisema mradi huo wa hospitali ya mama na mtoto utasimamiwa kwa karibu na taasisi hiyo lakini haitakuwa jukumu lake pekee bali wananchi wote bila kujali itikadi zao.
Elifuraa alisema tayari mchora ramani amekwishapatikana na kupatiwa jukumu la kuandaa michoro lakini pia ArDF wanafanya mawasiliano na madaktari bingwa ili waweze kutoa mawazo yao ili jengo liwe la kisasa zaidi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless Lema alisema kwamba tukio hili la leo ni faraja sana kwake na ni jibu kwa wote walioandika ama kuzungumza mabaya dhidi yake siku za nyumba kwamba alishakabidhiwa viwanja hivyo na kuviuza, kitu amcho amedai leo imedhihirika ukweli na uongo ni upi.
Lema ameahidi kutimiza kila ahadi aliyowaahidi watanzania hususani wakazi wa Arusha na kwa kuazna na hospitiali ya kina mama na watoto amedai mipango iliyopo ni mpaka kufikia mwezi Juni mwaka huu jengo la Utawala la hospitali hiyo litakuwa tayari.

DSCN7652Mh Mbowe na baadhi ya viongozi wa Chadema, Wawakilishi wa Mawala Advocates, Madiwani wa Chadema, Waandishi wa Habari na wananchi wakikagua mipaka ya shamba hilo
DSCN7649
DSCN7633Baadhi ya waandishi wa habari na mabloga wakiwa kazini
DSCN7639Mkurugenzi wa Mawala Trust, Bw Godfrey Mawalla akimkabidhi Mh Lema hati za viwanja hivyo vyenye thamani ya shilingi miliono 480. Ilielezwa kuwa lengo la matumizi ya viwanja hivyo ni kwa ujenzi wa hopsitali hiyo ya kuhudumia kina mama na watoto na si vinginenvyo.
DSCN7635Mwakilishi mwingine wa kampuni ya Mawalla Advocates na Mawalla Trust akitoa salamu
DSCN7620Mh Mbowe akiwasili shambani hapo
DSCN7628Mratibu wa maswala ya wanawake Chadema Arusha, Bi Cecilia Ndosi akizungumza katika hafla hiyo, akiwakilisha kina mama ambao ndio walengwa wakubwa wa mradi huo, bila kusahau watoto wao.
DSCN7627Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA Jijini Arusha, akitoa neno kwa niaba ya madiwani wenzake
DSCN7630Mwenyekiti wa Mfuko wa Maendelo Arusha (ArDF), Bw Elifuraha akitoa ufafanuzi kuhusiana na mradi wa hopsitali ya mama na mtoto inayotarajiwa kujengwa eneo la Burka chini ya usimamizi wa taasisi hiyo
DSCN7632
DSCN7611Baadhi ya waandishi wa habari wakiingia eneo la shughuli rasmi ya makabidhiano hii leo