KIJANA ACHOMWA KISU AKITOKA KUPATA STAREHE ZA MWISHO WA WIKI


Kijana Godfrey Masharo mkazi wa mjini Iringa akivuja damu baada ya kuchomwa kisu kifuani na watu wasiofahamika usiku wa leo wakati akitoka kujirusha disco

Hapa akivuja damu akiwa nje ya kituo cha polisi kabla ya kupelekwa hospitali ya mkoa wa matibabu zaidi

Hivi ndivyo alivyochomwa kisu kifuani.

WATU wasiofahamika wamemvamia na kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani mkazi wa mjini Iringa Godfrey Masharo (pichani) .


Tukio hilo limetokea jana usiku majira ya saa 11 alfajiri wakati kijana huyo akitoka kujirusha katika kumbi za starehe mjini hapa.

Akizungumza kwa tabu kijana huyo anadai kuwa watu hao watatu ambao hawafahamiki kwa majina walimvamia na kumchoma na kitu hicho chenye ncha kali kifuani na kukimbia .

Alisema kuwa tukio hilo limetokea eneo la Miyomboni barabara kuu ya Iringa -Dodoma jirani na jengo la Hazina Ndogo ya mkoa wa Iringa .

Hata hivyo alisema kuwa msaada wake ulitoka kwa wasamaria wema ambao walimkuta eneo hilo akiwa ameanguka kwa kupoteza fahamu na kukimbizwa katika kituo cha polisi kabla ya kupelekwa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi .